Advertisements

Monday, July 4, 2016

BODI YA MIKOPO(HESLB) YAKANUSHA TAARIFA ZA KUISHIWA FEDHA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu HELSB imekanusha vikali taarifa iliyonea katika mitandao ya kijamii kuwa imeishiwa fedha za kuwalipa wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu mwaka huu.

Taarifa ya kuishiwa fedha ilienea katika mitandao ya kijamii ikidaiwa kuwa Taasisi hiyo muhimu ambayo ni mkombozi kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu hapa nchini imeishiwa fedha ndio maana fedha za mikopo zinachelewa kuwafikia.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano HESLB imebainisha kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji na zina lengo ya kuleta taharuki miongoni mwa wanafunzi suala ambalo halina ukweli wowote.

“Si kweli kwamba Bodi haina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.”Imesema taarifa ya Bodi hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.

No comments: