Advertisements

Wednesday, July 20, 2016

BODI YA UTALII YASISITIZA MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA

Bodi ya Utalii nchini imetoa taarifa kufafanua kuhusu mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.

Taarifa hiyo imekuja baada ya kutokea kwa kifo cha dereva wa kimataifa wa mbio za magari Guguleth Zulu, aliyefariki dunia wakati akipanda Mlima Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa ya bodi ya utalii kwa vyombo vya habari imekanusha taarifa iliyochapishwa na mwandishi wa shirika la AP kwamba milma huo upo Kenya.

‘’Tungependa kusahihisha habari za kupotosha kwamba mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,”

Aidha Bodi ya Utalii Tanzania imeandika barua kwa chombo cha habari kilichofanya makosa hayo na kutaka wafanye marekebisho.

Miezi michache iliyopita mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, Rose Mary Odinga akihutubia vijana nchini Marekani aliwaambia Olduvai Gorge ipo Kenya na baadaye alikanusha taarifa hiyo.

4 comments:

Anonymous said...

Tangazia nje ya nchi uwezo wa Mt Kilimanjaro. Siyo bra bra zisizoisha ukiwa Manzese umeshiba ugali.

Anonymous said...

Huu ugomvi wa kijinga sana. Hata wakenya wanatucheka. Wacha wadai wanavyodai. Hivi mtoto wa Kenya akidai mlima upo kwao kweli ni swala la taasisi nzima ya serikali kumjibu. Watanzania nao wajibu. Yaani watu wetu hawakerwi kujibu. Tunakuza madai ya kijinga na kupoteza muda wa Taaasisi zetu. Sisi tutangaze vivutio vyetu vikiwemo Kilimanjaro. Hayo madai mengine ya wajinga na wapumbavu ni ya kudharuliwa. Kama wanavyosema - if you argue with a fool people might not notice the difference. I am afraid TANAPA is are getting there.

Jay said...

Balozi wetu aliye Marekani anafanya nini ku rectify this nonsense? It's too much now.

Anonymous said...

Lkn wakenya wamezidi kututumia. Waelezwe kisheria. Sio huyo tu wakenya wanatabia ya kuwadharau watanzania tena wanatucheka na kutuita maxiwa lala kisa hatupendi shari. Wakenya acheni hizo Kilimanjaro ni ya Tanzania si ya Kenya.