Advertisements

Saturday, July 9, 2016

DOLE LA KATI LA MBUNGE MR SUGU LILILOSABABISHA AFUNGIWE BUNGENI

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' akiwaonesha wabunge wa CCM dole la kati Bungeni Dodoma hivi karibuni, kitendo ambacho kilitafsiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa ni tusi, hivyo kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao kumi vya Bunge. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

4 comments:

Anonymous said...

Kama si upuuzi kitu gani? Kama si ujinga kitu gani? Kama si ufedhuli na ubaradhuli kitu gani? Kama si ulimbukeni kitu gani? Kama si ukosefu wa malezi ya utotoni kitu gani? Kama si upumbavu wa mtu mzima kutojitambua ni kitu gani? Kweli? Yaani ndani ya bunge kutoka kwa mwakilishi wa wananchi anaenda kuonyesha ishara ya mwanamme kwenda kumvua nguo mwanamme mwenzake? halafu tunaambiwa hawa ni watu smart wanaopigania kushika dola na kuiongoza nchi yetu? Kwa upuuzi wa kiasi kama hiki siwezi kuilaumu serikali ya Magufuli hata kidogo kuzuia kuonyesha matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni kwani hapana shaka ni kuinusuru jamii hasa watoto na vijana kuiga tabia chafu na za kijinga kutoka kwa watu waliowaamini kuwa ni mifano yao hadi kuwachugua kuwa wawakilishi wao serikalini. Kwa kweli kitendo alichotenda Sugu ni upumbavu uliopindukia kwa kwetu hapa Marekani na sehemu nyengine duniani mbunge hawezi kutenda tendo kama lile bungeni halafu akasalimika kisiasa kwanza yeye mwenyewe mbunge binafsi uso wake angeuweka wapi mbele ya jamii anayoiongoza? Na kama bado ndugu Sugu anajidhatiti kuendelea na zamana yake ya ubunge baada ya hii kashfa basi hawatendei haki wapiga kura wake na anawachukulia kama watu rahisi sana (very cheap people) anaoweza kuwatumia kwa kupita juu ya migongo yao kwa maslai yake zaidi na kwa kweli hii si sahihi hata kidogo.

Mohamed Mtambo said...

Nisawa kufungia Matangazo ya Bunge. Kwani uupumbav + uhuni + ujinga + ulimbuken an ushamba. Ndio waliopo BUNGEN

Anonymous said...

Kama qualifications za mbunge ni kujua kusoma na kuandika haishangazi kuwa na wabunge wa quality hii.

Anonymous said...

annony 1 and 2. well said. Hawa wapinzani wanawaangusha wale walowapigia kura. it is a betrayal the voters should not forgive them at the next ballot. Ni kweli serikali ina kila haki ya kufungia matangazo kama mambo ndio hayo ya wendawazimu na ujinga as illustrated by Sugu and his camp has remained in silence. Nashangaa katika hili hakuna hata Mbunge wa Upinzani aliyelilaani. hayo sio maadili ya kiafrika. asituletee uhuni sisi.