Advertisements

Wednesday, July 13, 2016

KIWANDA CHA TWIGA CEMENT CHAPEWA MWEZI MMOJA KUREKEBISHA MFUMO WA UTOAJI TAKA

Kiwanda cha kutengeneza cement cha Twiga cement cha wazo jijini dare s Saalaam kimepewa muda wa mwezi mmoja kurekebisha mfumo wao wa utoaji taka ili kunusuru uharibifu wa mazingira na maisha viumbe hai.

Hayo yamesemwa Leo jijini Dar es Salaam na waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho.Mhe. Mpina amekitaka kiwanda hicho kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupima vumbi litokanalo na uzalishaji kiwandani.. ili kuona kama ni la kiwango ambacho si hatarishi kwa mazingira na viumbe hai vinavyozunguka maeneo hayo.

Maagizo hayo ya Naibu waziri Mpina yametokana na malalamiko ya wananchi wa maeneo jirani na kiwanda hicho yanayoeleza kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wakazi au majirani wa maeneo hayo hivyo, amemtaka muwekezaji huyo kuimarisha mahusiano baina ya kiwanda hicho na wananchi na kufanyia marekebisho kasoro zilizoonekana kujitokeza kiwandani hapo na kuwaasa wawekezaji wa kiwanda hicho kufanya kazi pamoja na kuheshimu sheria hususan za mazingira.

Kwa upande wa Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira Nemc kumeonekana kuwa na uzembe katika ufuatiliazi wa utekelezaji wa sheria za mazingira hasa kiwandani hapo, baada ya mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa baraza hilo bi Ruth Lugwisha kushindwa kujibu swali aliloulizwa na Naibu waziri Mpina kuwa ni lini Mara ya mwisho baraza hilo lilijiridhisha kwa kuchukua vumbi kiwandani hapo na kulipima ili kujua lina athari kwa kiasi gani kwa mazingira na viumbe hai.

Kwa upande wake Meneja wa Mazingira wa kiwanda hicho Bw. Bw. Richard Magoda amejitetea kuwa kiwanda kina mahusiano mazuri na wanachi kwani kimeweza kutoa misaada katika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na vyandarua na kuchonga barabara za baadhi ya mitaa.

Wakati huo huo viongozi wa serikali za mitaa Bw. Gration Mbelwa (mwenyekiti wa kata ya madale) na Atilio Maginga mwenyetiki wa serikali ya mtaa wa mivumoni..wametofatofautiana kwa kusema kwamba kiwanda kina mashirikiano mazuri na wananchi, wakati mwenyekiti wa kata ya madale akiwakilisha wanachi kwa kulalamika kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wananchi.

No comments: