Advertisements

Friday, July 22, 2016

MAALIMU SEIF KUTINGA ICC LEO

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim
By Fidelis Butahe, Mwananchi fbutahe@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati polisi wakisema wanasubiri jalada la Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad litoke kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) ili wamfikishe mahakamani kwa uchochezi, leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali.

Maalim Seif anakwenda kuwashtaki viongozi hao kwa madai kuwa, walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kisha kuwatesa, kuwakamata na kuwapiga wafuasi wa chama hicho bila makosa.

Mei 22 mwaka huu, chama hicho kilizindua ripoti yake ya uvunjwaji haki za binadamu Zanzibar wakati wa uchaguzi huo na kutangaza azma yake ya kwenda ICC kuwashtaki Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema jana kuwa mpango huo umekamilika na Maalim Seif ambaye yupo nje ya nchi kwa ziara ya kueleza alichodai ‘figisufigisu’ zilizotokea katika uchaguzi mkuu, ataweka wazi kila kitu kilichotokea na jinsi ukiukwaji demokrasia ulivyoshika kasi nchini.

3 comments:

Anonymous said...

Hivi CUF hawana wasomi ama wanasheria wakuwafahamisha taraibu za ICC?

Huyu anamdanganya nani ama ni mpumbavu kiasi hicho haelewi analolifanya kuwa ni mbio za sakafuni.

Ama ndio kuwapumbaza wanachama wake? Kweli wajinga ndio waliwao.

Hebu mtu achukue Statute ya ICC aone jinsi inavyoweza kuchukua kesi kutoka kwenye nchi. Huendi tu!

Ajabu na ujinga mkubwa huu!!

Anonymous said...

Hakuna kitu hapo, Maalim Seif anawaingiza CUF chaka.

Anonymous said...

Naona mzee maalim Seif anatafuta kila njia ku remain relevant ndani ya CUF.
Natumai hata yeye mwenyewe anatambua kuwa katika 4 core international crimes ambazo ICC wana deal nazo hakuna hata mmoja linaifunga serikali.