Advertisements

Wednesday, July 20, 2016

MADIWANI WA BIHARAMULO NA KYERWA WAFUNDWA KUHUSU MAADILI, RUSHWA NA UENDESHAJI MIKUTANO

MKUFUNZI katika Mafunzo elekezi kwa Madiwani, Lazaro Kasumbe Busiga kutoka Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) akitoa mada ya Kanuni na Taratibu za Uendeshaji wa Mikutano katika Serikali za Mitaa na panoja na mada ya Kanuni kuhusu Maadili ya Madiwani kwa madiwani wa Halmashauri za Biharamulo na Kyerwa mkoani Kagera leo.

Kasumbe ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo mkoani Dodoma, alisema lengo la mada hiyo ni kuwawezesha madiwani hao ambao Halamashauri zao zinaanza utekelezaji wa mradi wa PS3 Mkoani Kagera kujua taratibu muhimu zinazotumika katika kuendesha mikutano na shughuli nyingine muhimu za serikali za mitaa. Source: Father Kidevu Blog, Bukoba.
Mwezeshaji wa Mradi wa PS3, kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Manumbu Daudi akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi wa Watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoani Kagera, Joseph Mwaiswelo akitoa mada juu ya athari  zakutoa ama kupokea  Rushwa, vyanzo vya rushwa katika serikali za mitaa, Hatua zinazochukuliwa na taasisi kukabiliana na tatizo la rushwa na Mambo ya kuzingatiwa na Madiwani katika kupambana na rushwa.


Madiwani wengi waliilalamikia taasisi hiyo kutoakana na kuchelewa kutolea maamuzi baadhi ya malalamiko ya Rushwa pamoja na kukosekana kwa ofisi za TAKUKURU katika maeneo yao na kuwataka kufungua ofisi katika ngazi ya Kata.

Mwaiswelo alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kesi nyingi za Rushwa ni kukosekana kwa ushahidi hasa pale Mtoa taarifa anaposhindwa kufika kutoa ushahidi. 
Pia alisema lengo linguine ni kumpa Diwani ufahamu muhimu juu ya kanuni za Maadili ya Madiwani ili kumwezesha kuwa na mwenendo unaotazamiwa na jamii anayoitumikia katika maisha ya utekelezaji wa majukumu yake.


Mafunzo hayo yanamuwezesha Diwani kuainisha mahitaji muhimu ya uendeshaji wa vikao, kueleza maana na dhana ya akidi ya mikutano na vikao, kuainisha mambo muhimu wakati wa maandalizi ya mikutano pamoja na kumuwezesha diwani kuanisha taratibu za uundaji wa Kamati za kudumu.



Aidha kwa upande wa mafunzo juu ya Kanuni kuhusu maadili ya Madiwani yatamuwezesha diwani kuainisha kanuni za maadili ya madiwani , kuzingatia maadili hayo wakati wa utekelezaji wa majukumu yake na yatamfanya diwani kutambua mahusiano ya kiutendaji kati yake na watumishi wa halmashauri.

 Washiriki wakiuliza maswali mbalimbali kutokana na mada zilizo wasilishwa na wawezeshaji.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini mada hizo.
Wakuu wa Wilaya za Kyerwa, Kanali (Mstaafu) Shaaban Lissu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde (katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Wende Ng'ahala wakifuatilia mada hizo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 Washiriki wakifuatilia kwa makini mada hizo.
Maofisa wa PS3 wakiwajibika kuhakikisha mambo yanaenda vyema (picha ya juu) huku Wataalam wa Masuala ya Utawala wa Mradi wa PS3 wakifuatiia mijadala kwa umakini na kuitolea ufafanuzi.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini mada hizo.
 Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde akichangia hoja mbalimbali.
 

No comments: