ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 28, 2016

MAKALLA ATOA SIKU SABA KUONDOKA KWA MALORI YOTE YA MIZIGO JIJINI MBEYA YANAYOEGESHWA KINYUME NA TARATIBU


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Amos Makalla ametoa siku saba kwa Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuyaondoa magari yote ya mizigo yanayoegeshwa pembezoni mwa Barabara kuu kinyume na utaratibu wakati kuna vibao vinaeleza ni marufuku magari ya mizigo kuegeshwa maeneo hayo." Siwezi kuendelea kuona magari yamejazana hapa kuna vibao vinakataza lakini watu hawatii, madiwani mpo, viongozi mpo, Takataka zinazagaa Watendaji Mpo, Viongozi Tupo kuanzia leo Usafi wa Jiji letu ni Sehemu ya kipaumbele na kwa kuanzia magari yote ya mizigo ndani ya wiki moja yaondoke yapelekwe eneo lililotengwa "

Hayo ameyasema jana katika kikao cha pamoja na madiwani na watendaji wa jiji la Mbeya wakati wa kujadili Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Serikali (CAG) Kuhusu ukusanyaji wa Mapato amewataka Watendaji na Madiwani kudhibiti Mapato kwa kuhakikisha Mapato yote yanakusanywa kwa njia ya (Elektroniki). Aidha amewataka madiwani kukagua miradi ili miradi hiyo iliyojengwa ieandane na Thamani ya Fedha.

Baadhi ya madiwani na watendaji wa jiji la Mbeya wakifuatilia kwa makini mkutano.
Wapili Kutoka Shoto ni Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Mh. Amos Makalla, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mh. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu) Katika picha ya pamoja baada ya Mkutano Kumalizika.


No comments: