Advertisements

Wednesday, July 20, 2016

MAKAMU WA RAIS ATUNUKU SHAHADA NA STASHAHADA KATIKA MAHAFALI YA NNE YA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Mahafali ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi ambapo wahitimu 38 walitunukiwa Stashahada na Shahada ya Usalama na Stratejia.
Mahafali ya Nne ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi ya kutunuku Stashahada na Shahada ya Uzamili kwa wahitimu 38.
Wahitimu 17 wamefuzu katika kozi ya Stashahada ya Usalama na stratejia na wahitimu 22 wamefuzu kwenye Shahada ya uzamili ya usalama na statejia ambapo wahitimu kutoka nchi za Botswana ,Burundi, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, South Africa, Zambia, Zimbabwe na China .
Mheshimiwa Makamu wa Rais amewatunuku Shahada wahitimu wote na wale waliofanya vizuri kwenye kozi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa Chuo Cha Taifa cha Ulinzi ambapo wahitimu 38 walitunukiwa Stashahada na Shahada ya usalama na stratejia.Makamu wa Rais alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mahafali hayo.

No comments: