Kutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu, imefahamika.
Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.
Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.
Taifa Stars ina mchezo na jijini Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa. Wachezaji ambao Mkwasa aliwaita mapema wiki hii ni: Makipa:
Deogratius Munishi,
Aishi Manula,
Benny Kakolanya,
Mebeki:
Kelvin Yondani,
Aggrey Morris,
Oscar Joshua,
Mohamed Husein ‘Tshabalala’,
Juma Abdul,
Erasto Nyoni,
Viungo:
Himid Mao,
Mohamed Ibrahim,
Shiza Kichuya,
Jonas Mkude,
Ibrahim Jeba,
Mwinyi Kazimoto,
Farid Mussa,
Juma Mahadhi,
Hassan Kabunda,
Washambuliaji:
Simon Msuva,
Joseph Mahundi,
Jamal Mnyate,
Ibrahim Ajib,
John Bocco,
Jeremia Juma
No comments:
Post a Comment