Advertisements

Friday, July 1, 2016

MUME MIAKA 60 JELA KWA KUMLAWITI MKEWE MJAMZITO

By Mwemezi Muingo, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Kibondo. Mkazi wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Jaribu Obedi (26) amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuingilia kinyume na maumbile mkewe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Erick Marley alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambao bila ya kuacha shaka umethibitisha mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo.

Alisema ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwake na wanaume wengine wanaokusudia kutenda kosa kama hilo.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Mei 28 na 30 usiku katika Kijiji cha Kumuhama.

Alidai mshtakiwa huyo alimfanyia kitendo hicho mkewe huyo wakati kwa siku tatu mfululizo wakati akiwa na mimba ya miezi saba.

Alidai kitendo hicho kilimuathiri kiafya na kukosa uvumilivu, hivyo kutoroka na kwenda kutoa taarifa kwa dada yake anayeishi Mtaa wa Migombani mjini Kibondo.

Mwendesha mashtaka huyo alidai baada ya dada yake kupata taarifa hizo, alimpeleka katika ofisi za ustawi wa jamii kisha polisi na ambako alipewa fomu namba tatu PF3 ili kwenda kutibiwa hospitali.

1 comment:

Anonymous said...

Makubwa Tanzania,tabia chafu. Na kama kathubutu kuingilia mti wake mwenyewe wakati wa usiku kwa staili ya wizi basi mti wa jirani hauwezi ukapona.