Advertisements

Thursday, July 14, 2016

NGOMA AFRICA BAND JUKWAANI JUMAMOSI MJINI BAYREUTH,UJERUMANI

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band yenye makao yake kule Ujerumani,wanatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho Carebic Festival litakalo fanyika jumamosi hii 16 Julai 2016 mjini Bayreuth ,Ujerumani ya kusini ambapo wapenzi wa muziki watapata burani ya aina yake kutoka kwa bendi hiyo iliyofanikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani,kikosi cha Ngoma Africa band kinachoongozwa na mkuu wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kinadudumu katika gemu la muziki kwa takribani miaka 23 sasa na kuwekwa katika rekodi ya kimataifa kuwa ndio bendi ya kiafrika inayodumu kwa muda mrefu barani ulaya,rekodi ambayo miaka 70s ilishikwa na Osibisa band.
usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

No comments: