Advertisements

Friday, July 8, 2016

PHILANDO CASTLE AUAWA MINNESOTA BAADA YA KUSIMAMISHWA NA POLISI KISA TAA YA BREKI HAIWAKI

Polisi jimbo la Minnesota wameua Mmarekani mweusi  Philando Castile baada ya kumsimamisha kwa sababu ya taa ya breki ya gari alilokua akiendesha kutofanyakazi.

katika video iliyomuonyesha Diamond Reynolds ambaye ni rafiki wa kike wa Philando Castile alikua akirekodi tukio huku ikimuonyesha rafiki yake wa kiume  Philando Castile akiwa anavuja damu huku akijaribu kuelezea jinsi tukio zima lilivyotokea.

Kwa madai ya Diamond Reynold alipokua akielezea jinsi rafiki yake wa kiume alivyopigwa risasi na polisi, alisema alikua na mtoto wake kwenye gari wakati tukio likitokea. Polisi waliwasimamisha kwa kosa la taa ya breki kutokuwaka na wao kama raia wema walifuata sheria zinavyosema.

Baada ya kusimamishwa polisi aliwaelezea kwanini amewasimamisha wakati huo mikono yao ikiwa juu mahali ambako polisi wanaweza kuiona na baadae polisi waliomba wapewe leseni ya dereva na kadi ya usajili wa gari na wakati Philando Castile akijiandaa kutoa polisi aliyekuwepo upande wa dereva alipiga risasi zaidi ya moja kwa mujibu wa madai ya Diamond Reynold alisema polisi walimfyatulia risasi Philando Castile tano mfululizo huku polisi akimwambia usitikisike kitu ambacho Diamond Reynolds anapingana nacho kwamba utawezezaje kuchukua leseni mkuo wa nyuma bila kutikisika?. Huu ni uonevu wa Polisi dhidi ya watu weusi ndivyo alivyokua akiendelea kudai mwana dada huyo.

Kwa upande wa Polisi wanadai wamepata bastola ndani ya gari kitu ambacho Diamond Reynold hakielezei katika maongezi yake na kudai Philando Castile alikua sio mtu wa mitaani alikua anakazi yake nzuri tu

Rais Obama wa Marekani amesema mauaji ya kikatili ya watu wawili weusi raia wa Marekani yaliyofanywa na polisi kama mengine yaliyotokea tukio jipya ni jambo kila Mmarekani anapaswa kulichukia.Rais Obama amesema ubaguzi umesababisha imani ya jamii kupungua dhidi ya polisi.

Ukiangalia asilimia 30 ya weusi Marekani ndio waliouawa na polisi nchini humo na asilimia kubwa ikiangukiwa kwa weupe huku asilimia chache ikiangukia kwa Waspanishi na makabila mengine. Jambo kubwa ambalo limejengeka kwa weusi ni kuona wanabaguliwa na Polisi weupe kwa rangi zao na mara nyingi ukiangalia mauaji mengi hutokea pia kwa kutokuwepo na imani kati ya polisi na weusi wa Marekani huku kila mmoja wapo akihisi mwenzake ni hatari.

Weusi wengi wanasema unaposimamishwa na Polisi hasa mweupe jitahidi kuwa mwangalifu zaidi kwani polisi anakufikiria tofauti ukilinganisha na anapokua amemsimamisha mtu mweupe, kitu ambacho kinapingana na ukweli kwamba ukiangalia kwa undani, asilimia kubwa waliouawa na polisi inawaangukia weupe.


2 comments:

Anonymous said...

It hurts...Damn America

Turudi kwetu tu sasa

Anonymous said...

Harudi mtu ,tutabanana hapahapa kwa Obama,R.I.P