Advertisements

Wednesday, July 20, 2016

RICHARD KASESELA: RASILIMALI KUBWA NI BINADAMU, KONGAMANO IRINGA

Mkuu wa wilaya Mhe. Richard Kasesela akipokea kitabu toka kwa bwana Daniel El Noshokaty ambaye alikabidhi vitabu kwa kila mwananfunzi kwa ajili ya kujisomea.
Wananfunzi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya Mhe. Richard Kasesela (hayupo pichani)
Wanafunzi kutoka Highland wakimskiliza Mkuu wa wilaya Mhe. Richard Kasesela.
Picha ya pamoja.

MKUU wa wilaya ya Iringa Mhe, Richard Kasesela leo amefungua kongamano la Wanafunzi wa shule za sekondari kujadili Maendeleo na matumizi ya rasilimali. Kongamano hilo liliandaliwa na umoja wawalimu wa masomo ya Uraia CETA wakishirikiana na na KAS -taasisi ya kujerumani.

Katika hotuba yake mkuu wa wilaya alisistiza kuwa rasilimali kubwa inayotakiwa kufanyiwa kazi ni Binadamu. Alisema " binadamu akijengewa uwezo anaweza kubadilisha rasilimali hizi ziwe na faida kwa maisha yake na wengine". Mkuu wilaya alisistiza suala la nidhamu kama msingi wa maisha, upendo na udailifu vinalete mabadiliko katika maisha ya mwanadamu. 

Naye Mwakilishi wa KAS bwana Daniel El Noshokaty akimkaribisha Mkuu wa wilaya alisema Taasisi ya KAS imeanza toka mwaka 1964 ikiwa na kazi ya kuelimisha wananchi juu ya elimu ya uraia hapa Tanzania na imetoa vitabu vingi kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa elimu hiyo. Kwa Irimga wataendelea kulimisha wanafunzi watambue fursa zilizopo katika rasilimali nyingi. 

Kingamano la siku moja lilikuwana na mada zenye kutambua uwezo wa nchi katika kuleta thamani kwa rasilimali zilizopo Tanzania hasusan Iringa. Shule za Lugalo, St Joseph, Kleruu, Kwelu, Highland na Mkwawa zililishirki katika kongamno hilo

No comments: