Advertisements

Sunday, July 31, 2016

SAFARI YA MWISHO YA DJ RACHY KUTTY

Raphael Chambo  kwa jina maarufu ni Dj Rachy Kutty enzi ya uhai wake.
Kutoka kushoto ni Dj Sweet Francis, Dj Ebony M na Dj Young Jesse wakiwa nyumbani kwa dada ya marehemu Sinza karibu na Vatikani siku ya Jumapili July 31, 2016 tayari kumsindikiza mwezao marehu Raphael Chambo aka Dj Rachy Kutty katika safari yake ya mwisho.
 Kutoka kushoto ni Dj John Peter Pantalakis, Dj Seif Katunda, Dj Sweet Francis na Dj Ebony M wakipata chakula kabla ya kuelekea kanisani kwa ajili ya Ibada ya marehemu Raphael Chambo katika kanisa la Mt. Alban.

 Ndugu, jamaa na marafiki wakipata chakula nyumbani kwa dada wa marehemu Sinza karibu na Vatican kabla ya kuelekea kanisani.
 Gari lililobeba mwili wa marehemu.
 Dj Young Jesse (mwenye kipaza sauti) akitoa tangazo la msafara kuelekea kanisani.
 Madjs wa zamani wakiwa kanisani wapili toka kushoto ni Dj Young Jesse, Dj Fast Eddy, Dj Peter Moe, Dj Ebony M na Dj Seif Katunda.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiufuatilia ibada katika kanisa la Mt. Alban.
Ibada ikiendelea. 
Madj Sweet Francis na Dj Richie Dillon wakiwawakilisha madjs wenzao kuweka shada la maua kwenye kaburi alikozikwa marehemu Raphael Chambo.
 Madj wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu katika makabuli ya Buguruni Malapa, jijini Dar es Salaam.


No comments: