ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 3, 2016

SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AUNGA MKONO JUHUDI ZA KUWAKOMBOA WAPALESTINA


Mgeni Rasmi katika semina ya kitaalam iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambaye ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum, akitoa mada katika semina maalum ya wataalam mbalimbali iliyokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja swala la siku ya QUDS Duniani ambayo n i siku maalum ya kuwakumbuka na kupaza sauti kuwatetea wananchi wa Taifa la palestina ambao wamekuwa wakipata mateso makubwa kutoka katika Taifa la israel siku ambayo iliazimishwa Jana Duniani kote huku watu mbalimbali wakifanya matembezi ya kuonyesha kuguswa na swala hilo.

Akizngumza katika semina hiyo ya Wataalam iliyofanyika Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Karemjee Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amesema kuwa swala la maisha ya wananchi wa Nchi ya Palestina ni swala la wanadamu wote bila kujali itikadi za kidini hivyo ni Jukumu ya kila mwanadamu kusimama kuwatetea wananchi ambao wanaporwa ardhi yao na Taifa la Israel..

Ameongeza kuwa katika kuazimisha siku ya QUDS Duniani ni siku sio ya wapalestina pekee bali ni siku ya kuazimishwa na dunia nzima kwakuwa mateso wanayopata wanadamu wenzetu ni makubwa na hayavumiliki hata kidogo.
Balozi wa palestina nchini Tanzania HAZEEM SHABAT akizungumza katika semina hiyo ambapo amesema kuwa hadi kufikia sasa watu zaidi ya 48488 wamepoteza mahali pa kuishi tangu mwaka 1967 jambo ambalo limekuwa hatari sana kwa wanadamu hao ambao hawana hatia.



Balozi huyo amesema kuwa Ni wakati sasa wa mataifa yanayopenda haki likiwemo Taifa la Tanzania kuinuka kwa pamoja na kuungana ili kupigania Haki ya nchi ya palestina ili waweze kuachiwa Ardhi yao ambayo imekuwa inadhulumiwa na Taifa la Israel na kusababisha madhara makubwa likiwemo la maafa na unyanyasaji mkubwa kwenye ardhi yao.

Balozi wa Jamhuri ya watu wa IRAN nchini Tanzania MEHDI AGHA JAFAI akitoa mada katika semina hiyo maalumu ya wataalam mbalimbali iliyofanyika kwa lengo la kujadili kwa undani mgogoro wa nchi hizo mbili ikiwa ni jana tu dunia imeadhimisha siku ya QUDS Duniani.

Balozi huyo wa IRAN amesema kuwa kutokana na ukubwa wa tatizo hilo baadhi ya mabalozi waliopo nchini na wadau mbalimbali wa amani wamelazimika kuunda kamati maalum maarufuu kama TANZANIA/PALESTINE SOLIDARITY COMMETTE kamati ambayo ina jukumu la kusimama na kupaza sauti kuwatetea wapalestina ambao wanateseka kwa sasa.

Aidha amesema kuwa kumekuwepo na juhudi mbalimbali za mataifa makubwa likiwemo Taifa la Marekani kujaribu kukwamisha Juhudi za kuwasaidia wapalestina ikiwa ni pampja na kutolipa swala hilo kipaumele ila ameuhakikisha ulimwengu kuwa wapalestina wapo imara na hawakati tamaa katika kutetea amani na haki yao ambayo inataka kuporwa na mataifa mengine.

Meza kuu ikiongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, wakiendelea na semina hiyo Jijini Dar es salaam

Profesa ABDUL SHARIFU kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (pichani) akizungumza kuhusu historia ya mgogoro mkubwa baina ya Mataifa ya Palestina na Israel.


BAADHI YA MATUKIO KATIKA SEMINA HIYO.





Baadhi ya picha za matukio ya mateso nchini palestina



No comments: