Kwa niaba ya Mariam Hussein tunapenda kutoa shukran za dhati kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki
wote waliojitolea kwa hali na mali, wakati wa mapambano ya Saratani ya Tumbo.
Amefarajika sana kwa michango ya pesa, waliokwenda kumuona, waliompigia simu kumjulia
hali, na kwa waliomuombea Dua kwa Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi wakati anapambana
na Saratani ya Tumbo.
Mariam Hussein amefanyiwa upasuaji June 7, 2016 katika hospitali ya George Washington
Memorial, Washington DC kuondoa uvimbe wa saratani kwenye tumbo na sasa hivi yuko
nyumbani anaendelea vizuri na recovery. Tunamshukuru Mungu kila kitu kimekwenda sawa.
Bado yuko kwenye uangalizi wa madaktari wake na ataendelea kutumia dawa za kusaidia kuto
kurejea kwa saratani mpaka watakapoamua kuwa hazihitajiki tena.
Tunaombwa tuendelee kumuombea dada yetu kwani maombi yetu bado yanahitajika.
Tunapenda kuchukua fursa hii kuwajulisha pesa tulizopokea kutoka kwenu kumsaidia wakati wa
mapambano haya :-
Go Fund Me $8,700
Harambee $4,300
Waliotuma direct $1,500
Jumla $14,500
Mwenyezi Mungu atuzidishie imani, upendo, maelewano na ushirikiano.
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
Asanteni sana.
Kwa Taarifa Zaidi
Asha Hariz 703 624 2409
Edima Elinewinga 202-459- 1217
No comments:
Post a Comment