Advertisements

Tuesday, July 12, 2016

TGNP MTANDAO YAWAFUNDA MADIWANI KWA LENGO LA KUWAJENGEA UWEZO KUHUSU BAJETI NA USAWA WA KIJINSIA

 Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bi Lilian Liundi akifungua mafunzo ya siku tano ya madiwani mbalimbali kutoka Tanzania mafunzo ambayo yana lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya Bajeti ya Tanzania na hususani kuichambua kwa mlengo wa kijinsia ili waweze kuwasaidia wananchi wanaowaongoza.
 Akifungua mafunzo hayo Liliani Liundi amesema kuwa lengo la TGNP ni kufwatilia na kunoa uelewa wa viongozi hao kuhusu maswala mazima ya bajeti ikiwa ni pamoja na kufwatilia jinsi bajeti inavyotoka na kutumika hususani bajeti yenye mlengo wa kijinsia ambayo amesema ni bajeti ambayo inapanga Rasilimali kulingana na makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii zetu alkisisitiza kuwa itakuwa ni bajeti ya haki kwa wananchi wote.

Zaidi ya madiwani 20 kutoka katika kata mbalimbali nchini Tanzania wameanza kupatiwa mafunzo ya siku tano yakiwa na lengo la kuwaongezea uelewa kuhusu dhana ya bajeti kwa ,mlengo wa kijinsia na matumizi yake katika kutengeneza mipango na bajeti kupitia nafasi walizo nazo.

Mafunzo hayo maalum yamefanyika Jijini Dar es salaam ambayo yameandaliwa na mtandao wa jinsia nchini Tanzania TGNP na kuwakutanisha madiwani kutoka katika kata tofauti hapa nchini ambapo yamefunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Mtandao huo Bi Lilian Liundi.

Amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha viongozi hao kutambua haki mbalimbali za makundi katika jamii katika Bajeti ya Tanzania na kuwajengea uwezo mkubwa wa kiuongozi hususani kuitumia Bajeti hiyo katika kuwasaidia wananchi hususani makundi yaliyopo katika jamii zao.
Baadhi ya madiwani ambao wamezngumza na mtandao huu juu ya mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yamekuja katika wakati muafaka ambao bajeti ya Tanzania imesomwa na sasa ni kazi ya viongozi wa ngazi za chini ambao ndio wanaokwenda kuitumia bajeti hiyo hivyo wameshukuru sana waanzilishi wa mafunzo hayo kwa kuwa yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi kila siku.
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia yanayoendelea kwenye semina 
Afisa Program uchambuzi na Machapisho kutoka TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba akitoa mada mbele ya madiwani waliofika kwenye semina ndani ya ukumbi wa TGNP Mtandao.
Mh. Adam Said ambaye ni diwani akichangia mada
Afisa Programu mwandamizi wa Ushawishi na utetezi kutoka TGNP Mtandao, Bi. Anna Sangai akitoa elimu kwa baadhi ya madiwani waliofika kwenye semina ya lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya Bajeti ya Tanzania na usawa wa kijinsia
 Baadhi ya waheshimiwa madiwani kutoka kata mbalimbali za Tanzania wakichangia mada katika mafunzo ya siku Tano iloandaliwa na TGNP Mtandao jijini Dar es salaam
 Maneja wa Programu ya Ushawishi na Utetezi, Grace Kisetu akitoa semina  akitoa mada mbele ya madiwani waliofika kwenye semina ndani ya ukumbi wa TGNP Mtandao.
Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakijadili jambo wakati wa semina ya madiwani iliyoandaliwa na shirika hilo

No comments: