Maneja wa Programu ya Ushawishi na Utetezi, Grace Kisetu akizungumza jambo kwa wanachama wa mtandao wa Itifaki ya kijinsi waliokutana kupitia mkataba wa nyongeza wa Maendeleo na jinsia wa SADC.
Mwezeshaji kutoka Sung Consultancy Firm Bw. Husein Sengu akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka asasi binafsi na za kiserikali katika ukumbi wa Seashells Jijini Dar.
Baadhi ya wadau kutoka asasi mbalimbali wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa kuhusu mkataba huo wa hiari ambao unatarajiwa kusainiwa na marais wa nchi wanachama wa SADC
Baadhi ya wadau kutoka asasi mbalimbali wakichangia mada
MTANDAO
wa jinsia nchini (TGNP) kwa kushirikiana na Asasi wanachama wa mtandao wa
Itifaki ya kijinsi wamekutana kupitia mkataba wa nyongeza wa Maendeleo na
jinsia wa SADC wa mwaka 2015
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika mkutano huo ulioshirikisha asasi na wadau
mbalimbali pamoja na wawakirishi kutoka serikalini, Meneja wa Ujenzi wa nguvu
ya pamoja wa TGNP, Grace Kisetu alisema warsha hiyo inalenga kutoa makubaliano
ya mkataba huo.
Alisema
kupitia mkataba huo wa hiari ambao unatarajiwa kusainiwa na marais wa nchi
wanachama wa SADC August mwaka huu utaondoa baadhi ya sheria ambazo zinaonekana
kukinzana.
“Ukiangalia
sheria ya ndoa za utotoni ya SADC ya mwaka 2008 inakinzana na sheria ya ndoa ya
Tanzania ya mwaka 2001 ambapo ya SADC inasema kuwa mtoto mwenye umri chini ya
miaka 18 aruhusiwi kuoa au kuolewa wakati ya hapa inasema mtoto wa umri wa
miaka 14 anaweza kuolewa kwa ridha ya wazazi au mahakama.
“Lakini
mkataba huu,kuhusu sheria hiyo imezuia kabisa na imeweka wazi kwamba hakutakuwa
na ndoa yoyote kwa mtu mwenye urmi chini ya miaka 18 jambo ambalo linaendena na
tafsiri yetu ya mtoto.
“Pia
kwenye mkataba umetamka wazi kwamba sheria zote hata zakwenye katiba ziweze
kutenguliwa na kupitia sheria kandamizi na zile zinazohusu ukatili wa kijinsia kuzitunga
mpya ili kuendana na sheria hii ya Kimataifa na ya Kikanda,” alisema Grace.
No comments:
Post a Comment