Hatimaye timu ya taifa ya Wales imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Ubelgiji kwenye michuano ya Uero inayoendelea huko nchini Ufaransa.
Wales wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 3-1 huku magoli yao yakifungwa na Williams kwenye dakika ya 30, Robson-Kanu dakika ya 55 na Vokes 85 huku goli la kufutia machozi la Ubelgiji likifungwa na Nainggolan kwenye dakika ya 13.
Hivyo basi timu hiyo ya Wales itakutana na timu ya taifa ya Ureno kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali huku fainali ya michuano hiyo ikitarajiwa kuchezwa Julai 10 mwaka huu.
Aidha michuano hiyo inaendelea leo kwa kuzikutanisha timu ya mabigwa wa dunia, Ujerumani itakayocheza na Italia.
No comments:
Post a Comment