Advertisements

Wednesday, July 13, 2016

WANAFUNZI 2,739 HAWAKUJITOKEZA KUHAKIKIWA NA HESLB

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Jerry Sabi (katikati) akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na kutoa taarifa ya awali ya zoezi la kuhakiki wanafunzi wanufaika wa mikopo ya wanafunzi lililoanza Mei 30, 2016 na linaloendelea katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa (aliyesimama) akitoa utambulisho wa Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kabla ya kuanza kwa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Julai 13, 2016 katika ofisi za Bodi zilizoko Mwenge jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Jerry Sabi (kushoto) akiongea na waandishi kadhaa wa habari mara baada ya kumaliza Mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na kutoa taarifa ya awali ya zoezi la kuhakiki wanafunzi wanufaika wa mikopo ya wanafunzi linaloendelea katika vyuo vya elimu ya juu nchini.


WANAFUNZI 2,739 hawakujitokeza kuhakikiwa katika zoezi la uhakiki wa wanafunzi kwenye Taasisi za elimu ya juu nchini  lilifanywa na Timu maalum iliypoundwa na Bodi ya Mikopo kuanzia tarehe 30 Mei, 2016 ambapo hadi sasa zoezi hilo linaendelea. 

 Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Jerry Sabi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa Katika zoezi la uhakiki wa wanafunzi jumla ya taasisi 26 zimehakikiwa, ambapo uchambuzi wa taasisi 18 umekamilika.

Amesema zoezi la kuhakiki wanafunzi linaendelea katika vyuo mbalimbali hapa nchini wataza na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yosefu, Chuo cha Biashara – Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Mwenge, Chuo cha Biashara - Dodoma na Chuo Kikuu cha Ushirika - Moshi.


Pia Bodi ya Mikopo imetoa wito kwa wanafunzi wote ambao hawajahakikiwa kujitokeza haraka ili wahakikiwe kabla ya kuhitimisha zoezi hilo.

No comments: