Advertisements

Thursday, July 28, 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHI MH:MWIGULU NCHEMBA ATUA MGODI WA NYAMHUNA UNAODAIWA KUTESA NA KUUA MTANZANIA MMOJA,AWAKAMATA WAHUSIKA(WACHINA NA WATANZANIA) WANAOSADIKIKA KUHUSIKA.

 waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba hii leo amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro-Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni watanzania.
Takribani wiki moja sasa kumekuwa hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.

Imemlazimu waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao kupitia wizara ya mambo ya ndani kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa watanzania.
 kijana akoinyesha majeraha aliyopata kutokana na mateso.Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la mtanzania kuteswa na huyo mwajili wake kipigo kilichopelekea kupoteza fahamu na sio kifo.
Hatua za awali mwigulu alizozifanya ni kwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ameshitakiwa na mwajili wake kwa kosa la wizi lililopelekea yeye kupigwa.


Katika mahojiano ya waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo,Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye mhanga wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na wakati yupo hapo gerezani.
Katika hali hiyo ilimlazimi Mh.Mwigulu kwenda mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwaajili ya kutambua waliofanya vitendo hivyo vya kinyama.Katika oparesheni hiyo, kijana  aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na mchina mmoja walioshirikiana kumpiga,kumtesa na kumjeruhi.Kufuatia utambuzi huo na maelezo ya wahusika,Nchemba akaagiza wahusika wakamatwe mara moja na ameondoka nao kwa hatua zaidi za kisheria.

Katika hali nyingine ya kusikitisha,Mwigulu amebaini uwepo wa wahamiaji haramu raia wa china katika mgodi huo ambapo nyaraka za uhamiaji mkoa wa geita zinainesha raia 28 wenye vibali ndio waliruhusiwa kukaa kwenye mgodi huo,lakini katika operasheni ya kushitukiza aliyoifanya Mh.Mwigulu nchemba amebaini uwepo wa raia wa china zaidi ya 50 wanaoishi katika mgodi huo kinyume na sheria.Hivyo amemuagiza mkuu wa mkoa na timu yake ya uhamiaji kuhakikisha wote wasio na vibali wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria
picha kijana huyu akiteswa na mchina huyo.

2 comments:

Anonymous said...

hivi lini tutabadilika, mkuu wa mkoa yupo, mkuu wa wilaya yupo, wakuu wa polisi wa mkoa na wilaya wapo!!!! lakini mpaka mheshimiwa waziri aende ndio kazi ifanyike, mfyuuuu zao, fukuza wote kazi wanafanya kazi kwa mazoea hao!!!!

Anonymous said...

Nakusuhuru waziri kwa kuingila kati na kutofuata ukiritimba wa sheria kwa kumtoa na kuwakamata hawa watu haramu ambao pesa za migodi yetu ndio inayowafanya wawe na kiburi na kutesa raia wetu bila sababu.Nakuomba kwa kuwa umeshapata ushaidi kamili huyu mchina kibali chake kufutwe mara moja na yeye na wenzake wote waondolewe nchini mara moja iwe fundisho kwa raia yoyote wa nje akija nchini ahaeshimu sheria na watanzania kwa ujumla.Pia naomba uwaulize hao polisi kwa nini walimshikilia huyu kijana bila ya kutaka kufanya uchambuzi na kujua nanai mwenye makosa?Au nao wanashirikiana na haya wachina kunyanyasa raia? ukibaini hivyo fukuza hao polisi mara moja washike adabu.Nakuomba sana waziri toa onyo kwa raia wengine wa kigeni kwa kuwafukuza na kuwanyima kibali hawa wachin na pi wamlipe fidia huyu kijana.