Advertisements

Wednesday, July 13, 2016

YANGA WA MCHANGIA MSEMAJI WA SIMBA PESA YA MATIBABU


Wanachama na mashabiki wa Yanga,usiku huu wametua nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa
Simba, Haji Manara na kukabidhi mchango wao kwa ajili ya matibabu.
Wanayanga hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano waYanga, Jerry Muro na walimkabidhi Manara kiasi ya Sh 1,055,000 kama mchango wao.


Wiki iliyopita, Manara aliamka jicho la kushoto halioni. Pia jicho lake la kushoto halioni vizuri pia. Hivyo anatarajiwa kupelekwa India kwa ajili ya matibabu na safari yake huenda ikawa Jumamosi hii.Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi mbalimbali ya mitandao ya Wanayanga.

“Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni mdogo sana. Lakini ni
mkubwa sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana.

“Nyie sasa mmredusha zile enzi za Yanga na Simba ambao walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile. Msiba wa Yanga wanazika Simba, Yanga wanazika Simba. Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema Manara.

No comments: