Profesa Ibrahim Haruna Lipumba na wafuasi wake 10 wametimuliwa kwenye Chama cha Wananchi (CUF). Wengine wapewa onyo kali. Wabunge Magreth Sakaya na Mbunge wa Mtwara mjini nao wanadaiwa kuvuliwa uanachama.
Abdul Kambaya (Mkurugenzi wa Habari) naye kavuliwa uanachama.
Katika kikao hicho kilichofanyika Vuga katika ofisi za Chama hicho walikosekana wajumbe watatu ambao ni Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdelina Sakay, Abdul Kambaya na Masoud ambao inadaiwa walionekana wazi katika kushabikia vurugu ya mkutano wa wiki iliyopita.
“Tumefanya maamuzi magumu kuna wengine tayari tumewafukuza na wengine kuwasimamisha” kilisema chanzo chetu kimaja kilichokataaa kutajwa jina lake.
Chanzo kilieleza kuwa hali hakuwa rahisi lakini mwisho wa yoote walifikia maamuzi hayo kwa maslahi ya chama ili kupeleka mapambano mbele katika kudai haki ya ushindi ya uchaguzi wa Zanzibar uluiofanyika October mwaka jana.
Mkurugenzi wa habari wa chama hicho, Salim Biman alieleza kuwa hawezi kueleza chochote hadi leo Agosti 29 saa nne asubuhi ambapo watazungumza na waandishi wa habari ili kuweka hadharani yale yote yaliopitishwa katika kikao hicho.
1 comment:
Sasa nidhahiri CUF gonjwa kubakia kuwa chama cha Wazanzibari.siku si nyingi kitaangukia kwenye meza ya msajili wa vyama vya siasa kwa kukosa uhalali wa kuwa chama cha siasa nchini kwa kushindwa kutimiza masharti.
Post a Comment