ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 27, 2016

JELA KWA MENO 7 YA TEMBO

Image result for MENO 7 YA TEMBO
Mussa Mbeho ,Katavi.

MAHAKAMA ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imewahukumu watu watano kutumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kumiliki meno saba ya tembo yenye thamani ya shilingi milioni 149.

Akisoma shitaka hilo mahakani hapo wakili wa serikali Bw.Wankyo Simon amesema watuhumiwa hao walikatwa na jeshi la polisi wakiwa na nyara hizo agosti 14 katika kijiji cha kakese nje kidogo ya mji wa mpanda wakijianda kuvisafirisha.

Ameomgeza kuwa baada ya kukamatwa walihojiwa na kukiri kuwa vipande hivyo walikuwa wakivisafirisha kuelekea jijini Daresalaam kwa ajiri ya kuvipeleka nje ya nchi kuviuza huku wakijua kuwa kufaya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mahakama ilitoa nafasi kwa watuhumiwa hao kutoa utetezi wao ndipo watuhumiwa wakawa hawana la kujitetea huku baadhi yao wakitokwa na machozi kwa lengo la kuishawishi mahakama iwapunguzie adhabu

Akitoa hukumu hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Chingangwa Tengwa amesema kuwa mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili hivyo watuhumiwa wote watatumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojishughurisha na biashara hiyo bila kuwa na kibali cha serikali.

Aidha waliohukumiwa kifungo hicho ni Justini Baluti (45),Boniface Hoza(33),Elias Hoza(17),Credo Gervas(27) na Sadock Masamba(43) wote wakiwa wakazi wa mkoa wa katavi

Mara baaada ya kutolewa kwa hukumu hiyo mahakamani hapa Gazeti hili likazungumza na wakili wa serikali bwana Wankyo Simon kuhusu hukumu hiyo ndipo akesema kuwa ameridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama kwa sababu yamezingatia vifungu vya sheria na haki imetendeka.

Kwa upande wake wakili wa utetezi wa watuhumiwa hao Bw.Elias Kifunda amesema kuwa wateja wake hawajaridhishwa na hukumu hiyo hivyo wanatarajia kukata rufaa ili haki itendeke vizuri.

Mwisho.

No comments: