Advertisements

Thursday, August 18, 2016

KASESELA AKUTANA NA MASELA KIHESA

katika kupunguza kasi ya uhalifu na kuwawezesha vijana wa Iringa Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alikutana na vijana wa kijiwe cha Kihesa. Ambao wengi wao wanajishughulisha na kuosha magari na kuwaomba kusiadiana naye katika kutokomeza udokozi. Vijana hao walimuomba mkuu wa wilaya mashine ya kuoshea magari ambayo aliwahidi kuwatafutia ndani ya siku 2 ili mradi wajiunge kwenye kikundi na wafungue akaunti benki. Vijana hao walimsukuru sana mkuu wa wilaya na kuahidi kuwa watiifu wa sheria na kuchapa kazi. Kikundi hicho kina vijana 25.

No comments: