Advertisements

Thursday, August 18, 2016

PEPO WA BONGO DANSI KAWAGANDA WASHABIKI ULAYA

Utamu wa muziki wa dansi wa kiafrika umegeuka kuwa pepo asiye sikia
ubani wala uvumba mbele ya washabiki wa muziki wa kiafrika kule ughaibuni,kwa takribanimiaka 23 sasa Ngoma Africa band imekuwa katika medani ya muziki katika majukwaa ya kimataifa kule ughaibuni na kufanikiwa kujizolea umaarufu kwa kuwanasa washabiki wa kimataifa katika kila kona. urimbo wanaoutumia kuwanasa washabiki wao ni "Muziki wa dansi" au Bongo dansi kutoka uswahilini na jirani mwa afrika mashariki. bendi hiyo mashughuli iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake mwanamuziki mtanzania Ebrahim Makunja kwa majina ya usanii Kamanda Ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens, bendi ya Ngoma Africa band na muziki wake imegeuka kuwa pepo aliyewaganda washabiki wa kila umri na kila jinsia, na kuifanya bendi hiyo kujiwekea historia ya bendu pekee ya kiafrika katika majukwaa ya kimataifa ,bendi ambayo mara nyingine usababisha ulinzi kuwa mkubwa kila wanapotumbuiza.bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya utani na washabiki wake,majina kama vile FFU-Ughaibuni,aka "Viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kutoka "Special Planet Bongo land".

Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kinapokwea jukwaani kinakuwa na kazi moja tu hakuna kuremba remba bali kushambulia kwa muziki moto mpaka

washabiki wanachanganyikiwa.

usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

uungana nao at www.facebook.com/ngomaafricaband

jarida moja la ujerumani limeitaja bendi ya ngoma africa kuwa yenye mafanikio na imeshinda mapambano kwa kuwa bendi pekee ya kiarika kuteka soko la muziki ujerumani na ulaya som athttp://www.afrikaportal.eu/portraet-ngoma-africa-band/

No comments: