YCEE pichani juu ambaye pia hufahamika kwa jina la Oludemilade Martin Alejo, anatarajiwa kufika jijini Dar es salaam tarehe 28th Agosti 2016 , ikiwa ni sehemu ya ziara yake yenye lengo la kutangaza nyimbo zake ambazo ni Omo Alhaji, Jagabana' na nyinginezo. Ziara hiyo itaambatana na mkutano wa waandishi wa habari siku ya Jumatatu tarehe 29th Agosti 2016, ikifuatiwa na ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya habari kuanzia tarehe 29th Agosti 2016 mpaka tarehe 1 Septemba 2016.
Msanii huyo aliyepata umaarufu kupitia wimbo wa ' Jagaban ' na ' Omo Alhaji ' amedhamiria kuungana na mashabiki, wazalishaji wa muziki na wasanii mbalimbali hapa nchini ili waweze kujenga mahusiano imara zaidi.
Pamoja na hayo amesema kuwa, anayo shahuku kubwa juu ya ziara yake kwani hii ni mara yake ya kwanza hapa nchini."Nina hamu sana ya kukutana na mashabiki wangu wa Tanzania, kwa sababu upendo wanaonipa kupitia mitandao ya kijamii ni wa ajabu na nina furaha sana ya kukutana na watu wapya " , alisema.
Baada ya ziara yake nchini Tanzania , YCEE ataenda nchini South Africa kuendelea na ziara yake yakukuza na kutangaza muziki wake, na anatarajia kuachia orodha ya nyimbo mpya baadaye mwaka huu utakao fahamika kwa jina la ‘The First Wave'.
Msanii huyo wa Omo Alhaji 'YCEE' pia ni miongoni mwa wasanii wanaopenda kusaidia jamii kwa kuwafikia vijana wa kiafrika katika masuala ya maendeleo na michezo.
Hivyo katika ziara yake hapa nchini YCEE atatoa msaada wa fedha kwa kituo cha masuala ya umaskini na ukosefu wa upatikanaji wa elimu kwa watoto wa mitaani Kigamboni. Kigamboni Community Center (KCC) , ni kituo kinacho shughulika na masuala ya kutokomeza umaskini, huku kikijikita katika kutoa elimu ya chekechea na msingi kwa watoto ambao wako mbali na upatikanaji wa elimu. KCC pia hutoa fursa nyingine za kujifunza kwa vijana wa Kigamboni, na pia hutoa elimu ya jamii, madarasa ya kuendeleza vipaji na mafunzo ya ufundi stadi. YCEE ameamua kuunga mkono kituo hiki kwa kwa sababu ya kujitolea kwao kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu kwa jamii.
LINKI ZA KUSIKILIZA NA KUTIZAMA NYIMBO ZAKE
Download link for Jagaban (Audio)
http://bit.ly/2bbKpff
Download link for Jagaban (Video)
http://bit.ly/1ia65Hl
Download link for Su Mi (Audio)
http://bit.ly/2b9IAR3
Download link for Su MI (Video)
http://bit.ly/2bIOjcy
Download link for Omo Alhaji (Audio)
http://bit.ly/2bYViCn
KUHUSU YCEE
Akifahamika zaidi kwa jina analotumia jukwaani ambalo ni YCEE, Oludemilade Martin Alejo kama ilivyoelezwa na BellaNaija ni msanii maarufu Nigeria. Alianza kazi yake ya muziki mwaka 2012 kama msanii chipukizi kabla ya kusaini mkataba na Tinny Entertainment.
Hata hivyo baada ya kupata nafasi ya kusoma Biokemia katika chuo kikuu cha Lagos aliacha kujishughulisha na masuala ya muziki kwa muda wa miaka miwili mpaka 2015. Alirudi tena katika ulimwengu wa muziki na wimbo wake wa 'Jagabani' na 'Condo' akishirikiana na Patoranking ambao ulimpandisha chati zaidi na kuteuliwa kushindania tuzo za 'Ushirikiano wa Mwaka ' na ' Video bora ya mwaka' kwenye 'Nigeria Entertainment Awards' huko New York.
YCEE alipata umaarufu kimataifa mara baada ya kuteuliwa kushiriki katika mchakato wa ‘Revelation of the Year’ katika tuzo za muziki za MTV Africa Music Awards 2015 , na kuteuliwa tena katika tuzo za ‘Best Artist in African Pop’ mwaka 2015 kwenye tuzo za 'All Africa Music Awards'. Pia alifanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo za ‘Rookie of the year’ kwenye The Headies mwaka huu.
Kwa sasa YCEE yupo chini ya lebo ya Tinny Entertainment, ambapo anaendelea kukuza muziki wake kibiashara kupitia wimbo wake mpya 'Sun mi' ambao ni remix ya ' Condo ' akishirikiana na Khuli Chana wa Afrika Kusini, KiD X , sambamba na DJ Consequence aliyeshirikiana nae hivi karibuni katika wimbo mwingine ' In Benz '
No comments:
Post a Comment