Advertisements

Wednesday, August 24, 2016

MSIBA DMV NA TANZANIA

Familia ya Bwana Deo Ruta wa Germantown, Maryland wanasikitika kutangaza kifo cha Baba mzazi wa Deo Ruta, Mzee Dr. William Isaiah Rutabanzibwa, kilichotokea August 22, 2016 Dar-es-Salaam, Tanzania.
Mipango ya mazishi inaendelea na familia ya Deo Ruta imeondoka kwenda Tanzania August 23, 2016 kwa ajili ya mazishi.
Kwa wale ambao wangependa kutoa rambirambi na mkono wa pole taarifa zaidi zitatolewa pindi familia itakaporudi toka Tanzania. Ila kwa sasa katika kipindi hiki kigumu sana kwa familia mnaombwa kuwakumbuka katika sala na maombi.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana na
Mrs. Tumaini Kaisi-Katule 1 301 433 3411
Mr. Pius Waricoy 1 240 353 1148
Mr. Tumaini Katule 1 301 433 1048

Mungu amlaze mahali pema peponi Mzee Dr. William Isaiah Rutabanzibwa. Amen!

1 comment:

Anonymous said...

Poleni sana wafiwa,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema AMEN