Advertisements

Thursday, August 18, 2016

RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU MPYA WA MKOA ARUSHA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo, Alhamisi, Agosti 18,2016.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho, Ijumaa, Agosti 19, 2016, saa 3 asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.

No comments: