Advertisements

Monday, August 1, 2016

SAFARI ZA MAJARIBIO ZA TRENI YA PUGU KUANZA LEO JUMATATU NA JUMANNE KUWA BURE

Huduma ya 2 ya treni ya Jiji kutoka Pugu kwenda kituo kikuu cha Dar es Salaam kuanza leo Jumatatu Agosti 01, 2016 saa 12 asubuhi.

Aidha taarifa Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL ) inafafanua huduma hiyo ya majaribio ya siku 2 yaani Jumatatu na Jumanne itakuwa bure kwa Wakazi wa vituo husika.

Vituo hivyo ni pamoja na Pugu stesheni, Mwisho wa Lami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana (Njia panda Segerea) na Karakata. Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi, SS Bakhressa, Kamata(Kariakoo) na Kituo kikuu cha reli Dar es Salaam.

Huduma hiyo itakuwa ya awamu 2 ya safari 3 kila awamu. Safari ya kwanza ya awamu ya 2 itaanza saa 9:55 Alasiri kutoka Dar stesheni.

Wito unatolewa kwa Wasafiri wa treni hiyo kuzingatia maelekezo ya Maafisa wa TRL watakaosimamia safari hiyo ya majaribio na kutoa ushirikiano kikamilifu.


No comments: