Advertisements

Monday, August 8, 2016

TRENI YA EXPRESS KUELEKEA KIGOMA MWISHO WA RELI

 Mmoja wa abiria akipanda ndani ya Behewa Dar es Salaam jana akielekea Kigoma kwa kutumia usafiri wa haraka  (EXPRESS), ambaye alifahamika kwa jina la Fatuma Kininga, aliushukuru uongozi mzima wa Shirika la Reli Tanzania,   kwa maamuzi yao ya kuanzisha usafiri huo na kuutaja kuwa ni mkombozi kwao.
Amesema kubwa hasa linalowasumbua ni upatikanaji wa tiketi ambao amesemani mgumu kiasi, Anawaomba wanaotumia usafiri huo kutunza mazingira bila shuruti kwa kushirikiana na wafanya kazi kuona ni mali yake, kutokanyaga viti, kula vitu na kutupa ndani ya mabehewa hayo, kuweka sheria kali na kuendelea kupewa elimu kila mara kwa abiria, na kila mmoja kumwelimisha mwenzake na kuwa mlinzi kwa mwenzake. Hayo aliyasema jana wakati alipokuwa ndani ya behewa Dar es Salaama. 
(PICHA ZOTE NA KAHMISI MUSSA)    
 Abiria wakiwa ndani ya Behewa tayari kuelekea Bara.

No comments: