Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
(Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa
Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu
Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai
amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa
ajili ya uchunguzi na matibabu.
Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya
akimweleza jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya
kumtembelea Mhe. Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa
Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
(Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa
CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini
Dar es salaam
Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakimwombea dua Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) ili aendelee
kuwa na afya njema ya kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu
walipomtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
(Kushoto) akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya
kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro akimuaga
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake
jijini Dar es Salaam. Viongozi wa CUF wamefika nyumbani kwa Mhe. Spika,
Job Ndugai kumjulia hali baada ya kurejea hivi karibuni akitokea nchini
India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO
1 comment:
Huyu Spika anaumwa nini? Mnona ni Spika wa nchi na Taifa halifahamishwi? Mhe. Kikwete alipoumwa alilitaarifu Taifa. Huyu kaenda India "kuchunguzwa" na kachunguzwa miezi mitatu! Kisha karejea nyumbani na misafara ya kumjulia hali haiishi!!! Ajabu sana. Uwazi na ulwell ungesaidia kwa vile naamini hata gharama za matibabu zililipwa na Serikali. Demokrasia ndivyo inavyohitaji. Hapa naona hata upinzani kwa kuwa wanafaidika na ukimya kama huu wote kimya!!! Bongo, unafiki mtupu.
Post a Comment