ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 5, 2016

Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli kuhusu TPA na TRA


MHESHIMIWA RAIS WANGU KIPENZI 
Rais wangu Magufuli, Pole na Kazi, Baada ya harakati za kutumbua majipu, changamoto ya uhaba wa sukari, wafanyakazi hewa kuna hili lingine linazidi kushamiri katika vichwa vya watanzania.

Nalo ni kupungua kwa mizigo Bandarini kunakopelekea kupungua kwa mapato. Hivi sasa kila mtu anajua kuwa Mizigo imepungua bandirini Mpaka tusio wataalam wa maswala ya bandari sasa tumeukariri wimbo huu. Mwanzoni wakuu wa bandari walizani ni hali ya mpito tu wakawa wanakanusha kuwa mizigo ipo ya kutosha . Sasa naona wameshtuka, wameona hali imezidi kuwa mbaya.

Mpaka mizigo ya nchi rafiki yetu kipenzi Rwanda imepungua kwa 47%. Mheshimiwa Rais, Pale Bandarini shida haikuwa kutokulipa Kodi na tozo. Shida ilikuwa Kodi tunazolipa haziendi serikalini. Ndio mana umesikia mfanyakazi wa TRA na Bandari alikuwa anahitaji kufanya kazi wiki Tatu tu kujenga ghorofa. Na Ndio mana ukasikia mfanyakazi mwingine anamiliki nyumba zaidi ya 100.


Shida sio kuongeza Kodi, shida Kodi hazikuwa zinafika serikalini. Ndio mana maafisa wako walikuwa wanaweza kupokea milioni 50 na kutoa risiti ya milioni 20. Nakushauri badili mfumo wa Kodi. Ijulikane wazi kwamba bidhaa fulani iliyonunuliwa kwa gharama fulani Kodi yake ni shilingi fulani. Tofauti na Sasa, Leo hakuna fomula ya Kodi, anakuja bwana Kodi anafungua kontena Kisha anakadiria yeye Kodi, na anachosema yeye ndio hugeuka kuwa sheria

Ndio mana kunakuwa na udanganyifu mwingi. Tunawaonea bure wajasiriamali kuwapandishia Kodi kwa kuongeza VAT kila kukicha. Shida ni maafisa wako. Waambie wapeleke Kodi serikalini. Ondoa utaratibu wa kukadiriwa na watu ambao unachochea rushwa na kupoteza mapato, weka mfumo wa moja kwa moja kuwe na bei elekezi. Weka Kodi ndogo na ya wastani ili uipate nyingi kwa wakati mfupi. Kuliko kuweka Kodi kubwa ambayo utaipata kidogo kwa wakati mrefu.

Ona sasa hata magari yenye plates number za majina yamepungua kusajiriwa na hayaonekani mtaani zaidi ya yale yaliyosajiriwa mwaka wa fedha uliopita. Hii ni Baada ya kupandisha kufikia milioni 10 kutoka 5. Ningekuwa mimi Ndio napanga hili ningeshusha Mpaka milioni 2 au 3 badala ya kupandisha.

Huo ni mfano tu Vinginevyo hizi kelele zitaongezeka kila siku kila leo. Ona Sasa kamati ya Bunge ya Bajeti inalalamika Mbunge Martha mlata wa CCM analalamika Mbunge Dalali kafumu wa CCM na mwenyekiti wa kamati ya viwanda na Biashara analalamika Marry Mwanjelwa wa CCM analalamika.

Hawa Ndio waliopitisha kwa vigeregere na shangwe kubwa Bajeti na kanuni mpya hizi bungeni lakini Sasa wamegundua kwamba walipotoshwa. Mheshimiwa Mkuu wa Kaya, Hili ni Taifa letu sote, hatupambani hatukomeshani, Tunashauriana. Tunashauriana namna bora ya kwenda kufikia nchi ya viwanda tunayoiota sote.

Mkuu, Taifa linaendelea kwa kujaribu, kutenda, na kukosea, wazungu wanaita try and errors. Tumelijaribu Hili la TPA na TRA naona tumekosea, tusilaumiane, tusitafute mchawi Mkuu. Tubadili Gia tusonge mbele. Taifa letu ni Hili Hili na hakuna wa kubadilishana nalo. Ndimi.

Habib Mchange
 Mwanachi. 
 0762178678

1 comment:

Anonymous said...

I agree let's learn from our mistakes.
Nobody knows everything