Advertisements

Tuesday, September 20, 2016

KILIMANJARO QUEENS BINGWA WA CECAFA WANAWAKE


Timu ya taifa ya soka la wanawake Tanzania bara, ‘Kilimanjaro Queens’ imefanikiwa kutwaa ubingwa wa baraza vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kuifunga Kenya kwa magoli 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa mjini Jinja nchini Uganda.
Mkongwe Mwanahamisi Omari aliifungia Kilimanjaro Queens bao la kuongoza dakika ya 26 kabla ya Stumai Abdallah kuzama nyavuni dakika ya 44 kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Christine Nafula aliifungia Kenya goli pekee dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kwenye mchezo huo wa fainali.

Safari ya Kilimanjaro Queens ilianza Septemba 9 ikiongozwa na kocha mkuu wa timu hiyo Sebastian Nkoma walikabidhiwa bendera ya taifa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera tayari kuelekea Jinja nchini Uganda baada ya kuhitimisha kambi ya siku chache mjini Bukoba.

Kabla ya kuelekea Jinja, Kilimanjaro ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0.

Wanadada hao wa Tanzania bara waliwasili Uganda wakiwa tayari kukipiga kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa wanawake katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania iliangukia kwenye Kundi B kundi lililokuwa na timu tatu (Tanzania, Rwanda na Ethiopia).

Ilianza kwa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Rwanda kisha ikatoka suluhu na Ethiopia na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwa matokeo ya kurushwa shilingi kufuatia kulingana pointi na Ethiopia.

Kwenye husu fainali wakakutana na wenyeji wa mashindano hayo timu ya Uganga ambapo Kilimanjaro ikafuzu hatua ya fainali kwa kuichapa Uganda kabla ya kuishinda Kenya na kutangazwa mabingwa wa CECAFA ya wanawake.
CREDIT.SHAFFIH DAUDA

No comments: