Advertisements

Tuesday, September 20, 2016

VEE MONEY KUJA NA TREY SONGZ


Msanii mwenye ‘title’ kubwa Afrika Mashariki,Vanessa Mdee Vanessa Mdee ‘Vee Money.

Stori: Boniphace Ngumije

BAADA ya msanii mwenye ‘title’ kubwa Afrika Mashariki, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kutajwa hivi karibuni kuwania tuzo kubwa za kazi na ubunifu zinazojulikana kwa jila la Loeries za Afrika Kusini kupitia video yake ya Niroge mwanadada huyo anatarajia kuibuka katika kolabo na mkali wa R&B duniani, Trey Songs.


Mkali wa R&B duniani, Trey Songs.

Vanessa na Trey watakutana kwenye msimu mpya wa Coke Studio International Week utakaoanza siku si nyingi na amefunguka kuwa mbali na kolabo watakayofanya hapo ni lazima atatumia nafasi hiyo kufanya kazi binafsi na mkali huyo kutoka Marekani. Mbali na Trey Songz , Vee Money atafanya wimbo na Patoranking kutoka Nigeria.
“Nahisi hii itakuwa nafasi ya dhahabu kufanya kazi na Trey, jambo ambalo namuomba Mungu mipango yangu iende sawa ili niweze kupiga naye kolabo kwa sababu ni msanii mzuri na anafun base kubwa duniani,” alimaliza Vee Money.

No comments: