Advertisements

Friday, September 2, 2016

KUZINDULIWA KANISA

TANGAZO
Wana wa Mungu wetu aliye hai, Amani iwe kwenu. Ninayofuraha kuwatangazia kuwa Swahili Lutheran Church itazinduliwa rasmi Jumapili September 11, 2016. Ibada itaanza saa tisa kamili mchana bila kuchelewa, wakati tuliopangiwa. Swahili Lutheran Church imesajiriwa rasmi katika jimbo la Maryland na kupewa Certificate Authentication Code: 5000000000818723
Nachukua nafasi hii kuwakaribisha wote. Nakuomba mkaribishe rafiki na jirani yako uje naye. Tutakuwa na mhubiri mgeni, The Rev. Dr. Joseph Bocko kutoka makao makuu ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Amerika, Chicago (ELCA African National Ministries Program Director.)
http://www.salemelca.com/BockoJoseph.pngC:\Users\John Mbatta\Pictures\Rev. John Mbatta.JPG
The Rev. Dr. Joseph M. Bocko Rev. John Z. Mbatta
Pia kutakuwa na waimbaji wa kwaya kutoka makanisa ya hapa inchini.
Ibada itafanyika kwa Anuani ifuatayo:
Living Faith Lutheran Church
1605 Veirs Mill Road (at Broadwood Drive)
Rockville, MD 20851


Kwa “Directions” wasiliana na Mch. John Mbatta kwa simu 703-863-2727
Amani  iwe kwenu. Mch. John Mbatta

14 comments:

Anonymous said...

Hivi ninyi wachungaji mtagawanyika mara ngapi. Kwanini msiungane muwe kitu kimoja Watanzania tujue mahali pa kukimbilia?? Kama hampendani ninyi kwa ninyi mtatushauri vipi sisi tupendane??? Nimeuliza hivyo kwa sababu lilianza kanisa moja la Umoja church, leo kuna makanisa zaidi ya matano yanayotoa huduma kwa lugha ya kiswahili. Wachungaji DMV mnamatatizo gani???

Anonymous said...

Hahaha

Anonymous said...

kwako mdau wa August 13, 2016 at 8:29 AM

kuna madhehebu tofauti, Lutheran, Episcopal(AKA Anglican), Roman Catholic, Assemblies of God, Non-denomination etc. yote haya yana miongozo tofauti, sasa unaposema liwe moja kwa hiyo madhehebu yote yawe na kanisa moja? ni sawa uwaambie wamarekani wote wawe na kanisa moja, au kwa waisilamu wa sunni waungane na shia waungane kisa wote ni waislamu. kwa mfano mimi ni m-katoliki, napenda nisali kanisa la katoliki na siyo la assemblies au non-denomination ingawa yote yanamwamini Mungu. Non-denomination laweza kuwa moja, lakini haya ambayo yako kwenye specific dhehebu hayaweza kuwa moja. kama kungekuwa na makanisa ya kiswahili ya Lutheran zaidi ya moja hapo unge-make sense.

Imani na dini/madhehebu ya watu waachie watu wenyewe

Anonymous said...

Mimi nadhani kuna kitu uroho wa kupata na tumeona makanisa mengi yanaibuka sana bila kuendelea. Yanaponza sana familia nyingi. Inafika pahala itushinde. Ninapita.

Anonymous said...

Kabla ya yote napenda kuweka wazi kwamba wachungaji wengi musipojitambua katika nafasi ya wokovu tuliopewa na Mungu wengi watapata hasara ya nafsi zao, asilimia kubwa ya wachungaji hawajui wito wao kama huduma, wala hawajui wanayemtumikia kingine hawajui tofauti kati ya huduma kwa Mungu na maadili ya kipagani, wengi wao wamejaa viburi na hupokea utukufu kuliko Mungu, wengi hupenda sifa na kuweka pesa mbele. Nashauri hivi, mchungaji zindua kanisa halafu shirikiana na wachungaji wengine kuunganisha utumishi mujenge umoja. Naelewa kuna wenye imani ya Angilikani, Lutherani, Morovian, pentekote, nk. Ni wakati sasa wa kulitazama wazo la kuungana. Wapentekote najuwa wanaweza kuwa wagumu kidogo, nimewahi kuwa kwa imani hiyo, lakini bado mnaweza kufanya kanisa moja kubwa. Kiasi aliyetoa comment hapo juu akashangaa.

Anonymous said...

Mchungaji hongera sana kwa upatikanaji wa kanisa, nasi tupo pamoja. Tupe nini cha kufanya na maandalizi ya ufunguzi wa kanisa letu. Tupo tulianza nawe na tutasimma na wewe pia, na mapepo yashindwa kwa jina la Yesu........

Anonymous said...

Tuko pamoja.

Anonymous said...

Mimi na my wife tunasubiri kwa hamu kubwa kanisa la kiinjili la Lutheran linazinduliwa. Hatukuwa na kanisa la kwenda, sasa kanisa langu litapatikana. Hongera mchungaji MBata. Niko pamoja nawe.

Anonymous said...

mdau wa August 15, 2016 at 3:05 PM...

"wengi hupenda sifa na kuweka pesa mbele"


PESA ZIPI?

Anonymous said...

hata Yesu alipigwa mawe sembuse sisi binadamu!

hongera sana baba mchungaji, hongereni sana kamati ya maandalizi, na karibuni wote tumsifu Mungu.

Anonymous said...

Naweka hii waz sote tunamfahamu mungu na ndie hutusaidia, lakin pia watumishi wamungu vaaeni utumishi wenu na kumcha mungu nafahamu wachungaji wengi wameowa na wanafamilia zao so jaman vaaeni utumishi wenu mliopewa na mungu na si kuweka macho mbele, pesa ni haki kutowa kwani bila pesa hakuna mafanikio hapo ila jamani watumishi wengine mhhh jaman jina la bwana libalikiwe! Hongera mchungaji mbatta bwana akuongoze ktk yote tuko nyuma yako tunakuombea,

Anonymous said...

Hongereni sana kwa hatua hii. Tutashirikiana pamoja bega kwa bega.

Mungu awabariki sana

Anonymous said...

ni habari njema. atukuzwe baba Mungu wa mbinguni.

Anonymous said...

Mch Mbata kwanza na kushukuru kwa kuchukua uamuzi wa kufungua kanisa la madhehebu ya kiluteri. mimi ni mluteri tangu kuzaliwa na kukuwa. dunia inatuchanganya sana na makanisa mengi yasiyojulikana madhehebu gani. ili mradi jina la mungu na la mwokozi wetu limetajwa hivyo ni kanisa.tunashindwa kujua linaanzaje na watoto wetu waende kimsingi gani. mimi nakuunga mkono sana sana na nitakuwepo na nitakuwa mkristo wa kanisa lako. nina hamu sana yakusikia vile vipengele vya nyumbani kama vile. keri eleiso na utukufu wa mungu juu mbinguni.... wewe ni qualified minister na umesoma na unajua unachofanya. mungu apewe sifa