Advertisements

Wednesday, September 14, 2016

MKUU WA WILAYA IRINGA AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela leo alifungua mafunzo ya Mgambo Kata ya Wasa na kata ya Kihanga karibu wana mgambo 170 wameanza rasmi mafunzo, pamoja na mambo mengine watajifunza uzalendo, mbinu za kivita,utawala na usalama wa raia. Mh Kasesela amesisitiza suala la usafi, kuacha ulevi, kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii na kuwa mwamminifu. Akimkaribisha Mkuu wa wilaya Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Iringa Lt. Col. Kitta alisistiza kuwa wanao jifunza mgambo wana fursa nyingi sana za ajira hivyo basi wajitahidi wote wamalize mafunzo. Mafunzo hayo mpaka sasa katika wilaya ya Iringa yapo Kata ya Wasa, Kihanga, Mboliboli na manispaa ya Iringa.

No comments: