Advertisements

Thursday, September 29, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ziara Wilaya za Buhigwe na Uvinza Mkoani Kigoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua dawa kwenye kituo cha Afya Uvinza wakati wa ziara yake hiyo mapema jana mchana Septemba 28.2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo mmoja wa wauguzi wa kituo cha Afya Uvinza wakati wa ziara yake hiyo mapema jana mchana Septemba 28.2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisikiliza maelezo ya viongozi wa kituo cha Afya Uvinza wakati wa ziara yake hiyo mapema jana mchana Septemba 28.2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo ya kitaalamunamna watakavyobadilisha wodi ya wanaume ili wajenge chumba cha upasuaji kwa viongozi wa kituo cha Afya Uvinza wakati wa ziara yake hiyo mapema jana mchana Septemba 28.2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na viongozi wa kituo cha Afya Uvinza (hawapo pichani) wakati wa ziara yake hiyo mapema jana mchana Septemba 28.2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo mmoja wa wauguzi wa kituo cha Afya Uvinza wakati wa ziara yake hiyo mapema jana mchana Septemba 28.2016
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya za Uvinza na ile ya Buhigwe na kutembelea Hospitali na vituo vya Afya ndani ya Mkoa huo wa Kigoma.

Akiwa katika kituo cha Afya cha Uvinza, Naibu Waziri ameweza kubaini mapungufu mbalimbali huku na kutoa maagizo kwa wasimamizi wake kuhakikisha wanafanyia marekebisho kasoro hizo kwa muda unaotakiwa kabla ya kuchukuliwa wahusika.

Miongoni mwa kasoro alizobaini ni pamoja na kuwa kituo hicho licha ya kuhudumia wananchi kama Hospitali ya Wilaya ya Uvinza, hadi sasa hakina sifa hiyo kwani hakina Chumba cha upasuaji, Maabara hisiyofuata utaratibu pia kutokuwa na maji kwa kituo hicho maji ambayo wanategemea kutoka kwa wagonjwa.

“Kituo cha Afya Uvinza, kinahudumia eneo lenye watu zaidi ya 59,000. Walipaswa kuwa 10,000 tu. Hakina maji, umeme Kwa sababu zisizo za kawaida. Hakuna Chumba cha upasuaji (Theatre), maabara ya kusuasua na dawa si za kutosha.

Nimewaagiza ndani ya miezi mitatu wawe wamekarabati eneo nusu la wodi ya wanaume kiasi cha kuweka Chumba cha Upasuaji. Pia wavute maji na kuweka matenki juu ili kuepukana na tabia ya kuagiza wajawazito kuja na ndoo za maji kituoni!. Nimewapa mwezi mmoja ili wavute umeme na kuanza kutumia Vifaa vyao Vya maabara.” Amesema Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo yake hayo kwa viongozi wa Serikali na wa Hospitali hiyo.

Aidha, kwa upande wa ziara yake katika Wilaya ya Buhigwe, Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi za wabia binafsi kwa kuweza kushirikiana na Serikali kwenye jambo la maendeleo huku akiwahakikishia uongozi wa Hospital ya Wasabato ya Heri Mission iliyopo eneo la Manyovu kuwa juhudi zao wanazitambua na suala la kuifanya Hospitali hiyo kuwa Hospitali teule ya Wilaaya zinashughulikuwa huku akiwataka kuzingatia sheria mbalimbali na mambo madogomadogo.

Dk. Kigwangalla ameutaka uongozi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanafanyia marekebisho ya barabara inayoingia Hospitalini humo pamoja na kuhakikisha wanajenga vituo zaidi vya Afya ili kuwafikia wananchi wake.

Dk. Kigwangalla yupo Mkoani hapa kwa ziara ya siku ambapo pia atatembelea Hospitali na vituo vya Afya vya Kigoma Mjini.

mwisho.

No comments: