Advertisements

Thursday, September 8, 2016

NHC YAMCHOMOA MPANGAJI WAKE MWINGINE KWA KUDAIWA MILIONI 96

Mfanyakazi wa Kampuni ya Kimbembe Auction Mart akitoa Samani za kampuni ya Centre Point Limited Mpangaji wa Shirika la Numba NHC Katika nyumba Plot Namba 2008/93 iliyopo Mtaa wa Indira Ghandhi jijini Dar es salaam kwa kushindwa kulipa kodi ya pango kiasi cha shilingi Milioni 96, tukio hilo limefanyika leo asubuhi.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimbembe Auction Mart wakitoa Samani za kampuni ya Centre Point Limited Mpangaji wa Shirika la Numba NHC Katika nyumba Plot Namba 2008/93 iliyopo Mtaa wa Indira Ghandhi jijini Dar es salaam.
Vitu mbalimbali vikitolewa ndani vikiwemo viti.
Baadhi ya vifaa mbalimbali vya kampuni hiyo vikiwa tayari vimetolewa nje.
Mmoja wa wanafamilia ambaye hakutaka jina lake litajwe akishuhudia tukio hilo wakati wafanyakazi hao wakiendelea kutoa vitu mbalimbali katika nyumba hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

Je mlikuwa wapi NHC wakati wote huo hadi kufikia milioni 96. Kwanza kabisa kabla ya kufanya hayo mkurugenzi aliyehusika atumbuliwe na wahasibu wa NHC nao majipu. Walikuwa wanafanya kazi gani. Imekuwa biashara ya kukurupuka tu! Kwa nini asipewe muda akalipa kiasi fulani na kuendelea kulomaliza? Mnatarajia kumpangisha nani kwa mtindo huu!?