Advertisements

Sunday, September 4, 2016

PAPA FRANCIS AMTANGAZA MAMA TERESA MTAKATIFU

Sasa hivi Mama Tereza anajulikana kama Mtakatifu Teresa wa Calcuta, baada ya kutawazwa rasmi na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis.
Leo maelfu ya watu wamejitokeza kushuhudia tukio hilo kubwa duniani la kutangazwa kwa kwa raia huyo wa Albania ambaye alifariki mwaka wa 1997.
Mama Tereza alianzisha shirika la hisani la kimishenari ili kuwasaidia walala hoi katika mtaa wa mabanda wa Calcutta nchini India.
Lakini wakosoaji wanesema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu waliokuwa wagonjwa na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu maskini wa kabila la Hindu nchini India kuwa Wakristo.
Sherehe za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel, zimehudhuriwa na wageni zaidi ya 1,000 wakiwemo wakuu wa nchi mbalimbali 13 na viongozi wa madhehebu hayo.
Ulinzi umeimarishwa wakati wa sherehe hizo. Mama Teresa aliyezaliwa mwaka 1910 katika taifa ambalo hivi sasa linajulikana kama Macedonia, alianza huduma ya utawa akiwa na umri wa miaka 16.
Ilikuwa ni kazi yake ya kuwasaidia wagonjwa na maskini huko Calcuta, India iliyompatia umaarufu mkubwa duniani kote, pamoja na kupokea tuzo ya amani ya Nobel.
Papa Francis amesema huruma aliyokuwa nayo Mama Teresa inapaswa kuwa mfano kwa Wakatoliki wote. Kutawazwa kwa mtawa huyo kunakuja miaka 19 baada ya kifo chake.

No comments: