Advertisements

Thursday, September 8, 2016

RC MAKONDA AKANUSHA TAARIFA ZA KUKAMATA WATU WANAKWENDA NYUMBA ZA WAGENI MCHANA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda amekanusha kauli zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amewaamuru polisi kufanya msako kwenye nyumba za wageni wakati wa mchana na kuwakamata wataokutwa muda huo.

Akizungumza na mtandao huu alisema hajawahi kutoa maagizo kama hayo, kinachofanyika ni Umbeya umbeya tu.

"Mimi kama Mwenyekiti wa ulinzi na usalama siwezi kutoa maagizo kama haya, kuna watu wanafanya kazi viwandani wengine usiku hivyo wanahitaji kupumzika mchana huwezi kuwazuia,
kinachofanyika ni Umbeya, siwezi kujibu hoja za kimbeya ni ujinga". Alisema Makonda.

1 comment:

Anonymous said...

Asante. Lakini kwa ujumla acha kutoa matamko mengi. Fanya kazi. Kuwanyima viongozi wenzako ndani ya jiji la Dar hata kama ninwapinzani hazina tija saidianeni kwa pamoja kuketa maendeleo ya jiji letu hata kama wengi watahamia Dodoma.
Pili hebu andaa kuondoa uchafu mwingi ulioko na ubovu wa barabara y a kutoka Kijiweni kupitia mtogore hadi magomeni inatia aibu maji machafu sana yamejaa pembezoni ukichangiwa na wamwaga maji machafu pia. Fanyeni kazi kwa pamoja acheni uCcm wala uCUF!