Advertisements

Tuesday, September 13, 2016

TANGAZO, TANGAZO, TANGAZO
Wapendwa,


Kama kuna mtu ana taarifa za huyu mtu hapa juu, naomba atoe taarifa rasmi kwenye dawati la Detective Matt Vendemio, Montgomery County Maryland Police, Patrol Investigation Unit 4th District , 2300 Randolph Road
Wheaton, Maryland 20902 / 240-773-5500 (front desk).


Tunaomba msaada wenu, mjitokeze kwani hadi sasa ameshachukua pesa zaidi ya $50,000 toka kwa Watanzania wengi walioko Marekani na baadhi ya viongozi toka Tanzania. Tayari kuna Watanzania aliowatapeli wameshafungua mashitaka dhidi yake na uchunguzi unaendelea toka state mabalimbali hapa Marekani.


Jina lake la halali ni WILLBROD FRANK LUKAMILWA . Amekuwa anajitambulisha kwa watu kwa majina tofauti tofauti. Kwa sasa kuna records kuwa ameshajitambusha kwa wengi kama Padri John, Padri Frank, Doctor Frank wa Georgetown Hospital, Pediatrician wa The Children Place, Mwanafunzi wa PhD wa Catholic University, Steve, Frank. Frank Stockman na John. Pia amekuwa akitoa maelezo kuwa ni mtu wa nchi tofauti kama Senegal, South Africa, Kenya, Congo na Belgium wakati ni Mtanzania wa mkoa wa Kagera.

Ametumia maelezo ya watu na mitandao kupata pesa toka kwa watu wengi walioko nje na ndani ya USA. Namba za simu za mkononi ambazo ameshatumia siku za karibuni ni
202-446-7747 na 202-867-2691.

Wilbrod alishashikwa mwaka huu June kwa utapeli pia, na bado anaendelea.Tunaomba ushirikiano wenu wa hali na mali, hata kuwagundua ndugu zake walioko Tanzania. Ni mwenyeji wa Bukoba, mkoa wa Kagera, Tanzania.


Huyu mtu ni hatari sana usimpe nafasi ya kuwasiliana na wewe kwani anatumia njia nyingi sana za utapeli (scamming schemes), tafadhali toa taarifa zako kama ni mmojawapo wa watu waliokwisha tapeliwa na huyu mtu.

http://www.nbcwashington.com/news/local/Police-Recognize-Arrest-Man-Right-After-Handing-Out-Wanted-Ads-383310751.html )

10 comments:

Anonymous said...

Huyu jamaa anasema ni doctor na anasaidia watu Georgetown Hospital kupata residency.... Mtu wa totoz kama wahaya wengine... na anapenda starehe sana mitaa ya DC

Anonymous said...

Za mwizi arobaini mwizi mkubwa!!!

Anonymous said...

Uwiiiii siamini!!!! alikutana na rafiki yangu akamwambia kuna gari la padre amekufa linauzwa chee kwa $3,0000 hadi leo huyo dada alishagraduate gari halikuonekana. Wacha Mungu aitwe Mungu kazi kwako ......Muda wako wa kusota umefika.

Anonymous said...

You should be careful what comes from your mouth or post on media, it shows how idiot you are.wahaya are very civilize and very successful people according to tanzania data,generalizing by tribe,gives me apicture how behind your with fact,goodluck .

Anonymous said...

Kasha kamatwa huyo yupo mikononi mwa Popoooo

Anonymous said...

Huyu mwanaume katepeli wanawake wengi,.kila akiopoa mwanamke anasema yeye Doctor,msomi,wahaya .

Anonymous said...

Wrong info... hajashikwa bado na polisi wanamtafuta. Someni post hii, kuna watu wamecopy maelezo bila kuonyesha ilikuwa posted lini online. Hii link ninya June 2016. As of leo sept 15, bado kuna watu wanazidi kujitokez ambao wametapeliwa kati ya June na end of August 2016


http://www.nbcwashington.com/news/local/Police-Recognize-Arrest-Man-Right-After-Handing-Out-Wanted-Ads-383310751.html

Anonymous said...

kwani wahaya siyo watu wa totoz, msinifanye niwataje kwa majina ;)
ndukiii...:)

Anonymous said...

We mhaya hapo juu hebu andika kiswahili

Anonymous said...

hii ni topic ya utapeli au ya wahaya!
wahaya mbona watu fresh tu, wasomi, wana maendeleo, wakarimu (hahahahahah).