Advertisements

Friday, September 30, 2016

VIFAA VYA SANGOMA VYANASWA UWANJA WA TAIFA, YANGA, SIMBA WATUPIANA MZIGO


Unaweza kusema utamu kunoga! Mechi ya watani, Yanga na Simba haikosi vituko. 


Kuna taarifa kwamba kuna vitu vinavyoashiria hali ya kishirikina vimekamatwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya mechi ya watani, Yanga na Simba, kesho.


Wakati vimekamatwa jana, lakini kila upande unatupa mpira kwa upande mwingine, kwamba ndiyo chanzo au unahusika.

Yanga wanasema ni Simba, nao Simba wanasema ni Yanga. Basi ili mradi siku zinasogea na inaendelea kuthibitika kwamba mechi hizo hasa za watani, watu ndiyo riziki zao.Watani wa jadi, Yanga Vs Simba wanakutaka kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lakini joto la mechi hiyo linazidi kupanda kwa kasi kubwa, hasa mitaani kwa watu kuvaa mavazi yanayoashiria wanasapoti timu gani.

Mfano, gari hilo aina ya VW ‘Bito’, mwenyewe anaonyesha kabisa ni shabiki wa Yanga au Wanajangwani na anajiamini kwamba, kesho wao ni kama kawa.

No comments: