Advertisements

Friday, September 30, 2016

VIONGOZI WA DUNIA WAHUDHURIA MAZISHI YA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAEL, SHIMON PERES


Askari wakiwa wamelibeba jeneza la mwili wa Shimon Peres
 Viongozi mbalimbali duniani wanajiandaa kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi ya kiongozi shupavu wa Israeli marehemu, Shimon Peres, aliyefariki Jumatano wiki hii.
Rais Barack Obama akizungumza jambo
Kuna ulinzi mkali katika eneo ambalo litatumika kwa mazishi yake, katika maeneo ya makaburi ya kitaifa mlimani Herzl mjini Jerusalem. Waombolezaji watajumuisha Rais wa sasa wa Marekani Barack Obama na Rais wa zamani Bill Clinton, aliyefanya kazi na Bw Peres katika mkutano wa mwafaka wa amani wa Oslo mwaka wa 1993.


Viongozi kadhaa wa Kipalestina pia watahudhuria mazishi hayo akiwepo Rais Mahmoud Abbas na mpatanishi mkuu wa zamani Saeb Erekat. Itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Abbas kuzuru Israel tangu 2010.
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton alikuwepo kutoa heshima zake kwa Peres

Maelfu ya Waisraeli walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Peres, ambaye maiti yake imekuwa nje ya majengo ya Bunge la Israeli, Knesset. Polisi wa Israel wamesema maafisa 8,000 wanatumiwa kudumisha usalama.

Mazishi hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika Israel tangu mazishi ya waziri mkuu Yitzhak Rabin, aliyeuawa na Myahudi 1995. Bw Peres alifariki Jumatano baada ya kuugua kiharusi kwa muda wa wiki mbili.

No comments: