Wachezaji
wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys,
wakijifua kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile
Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo.
Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2,
2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara
za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.
Kocha
wa Makipa wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 -
Serengeti Boys, Muharami Mohammed maarufu kwa jina la Shilton (wa pili kushoto)
akiwanoa vijana wake, Kelvin Kayego (kushoto), Ramadhani Kabwili (wa tatu
kushoto) na Samwel Brazio kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya
Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri
ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya
Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano
ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.
Purukushani
langoni ambako Dickson Job akiwa hewani akikoa hatari langoni kwake.
Shughuli
ilikuwa kati ya Kelvin Nashot Naftal (kushoto) na Zuberi Rashid Ada.
Madaktari
wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Dk.
Sheicky Mngazija (kushoto) na Gilbert Kigadye wakifuatilia kwa karibu mazoezi
ya timu kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda
wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys
inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la
Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko,
hapa jijini Brazzaville. Picha zote na Alfred Lucas wa TFF.
No comments:
Post a Comment