Advertisements

Tuesday, September 20, 2016

WANAFUNZI 15 WALIOCHARAZA VIBOKO WALIMU WASIMAMISHWA

WANAFUNZI 15 wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa Katavi wameamriwa kurejea nyumbani kwa wiki mbili kwa kosa la kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili akiwemo Makamu Mkuu wa Shule, Makonda Ng’oka ‘Membele’ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho.
Aidha, wanafunzi hao wanaodaiwa kuwa vinara wa mkasa huo wametakiwa kulipa faini ya Sh 20,000 kila mmoja wao na wametakiwa kuzilipa mara watakaporejea shuleni.
Taarifa kutoka shuleni hapo zinaeleza kuwa kikao cha Bodi ya Shule hiyo kilichokutana mwishoni mwa wiki, kilitoa adhabu hizo kwa wanafunzi hao ikiwataka wasionekane shuleni hapo kwa kipindi cha wiki mbili.
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Katavi, Ernest Hinju amethibitishwa kufukuzwa kwa wanafunzi hao akisema kuwa Bodi ya shule hiyo iliketi Septemba 16, mwaka huu shuleni hapo na kufikia maamuzi hayo huku akisisitiza kuwa maelezo zaidi atatoa baadaye.

Walimu hao wawili wameendelea kusisitiza kuwa kuwa hawako tayari kuendelea kufundisha katika shule hiyo huku wakisisitiza kuwa ni fedheha kwao kucharazwa viboko na wanafunzi wao wenyewe, huku mwalimu Gabriel Kambona akiachwa na ngeu kichwani. Mwalimu Kambona alidai kuwa haridhiki na adhabu waliopewa wanafunzi hao.

2 comments:

Anonymous said...

Yaani hao sio.wa kufukuzwa kwa wiki 2 tu ni kuwaachisha kabisa wakasome wanakowaamini waalimu. Lets be serious mwanafunzi anatakiwa kufuata taratibu sivyo kuna uongozi na kamati za shule!! I don't get it!!��

Anonymous said...

Kama huo uongozi wa shule hauchukui hatua yoyote je ? Wewe uliosema bora kuwaachisha kabisa shule, wewe ulisoma boarding school? Au nafikiri hujawahi kukumbana na walimu wa namna hii,ya kulawiti, maana mpaka yakufike na hupati msaada kutoka popote ndio utajua uchungu wake