WATUMISHI watatu wa serekali akiwemo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la
Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili
ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti
feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016.
Watumishi
waliofikishwa mahakamani hapo leo ni aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa
Kagera Amantus Msole,mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Kelvin
Makonda,Muhasibu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja wa banki ya CRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa.
Akiwasomea mashtaka yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya Bukoba
wakili wa serekali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao
wanashitakiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni watuhumiwa walikula
njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana
na jina la akaunti ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye no.015225617300 ,ambapo
wao walifungua akaunti yenye jina la KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba
no.0150225617300
Alilitaja shitaka la pili kuwa ni watuhumiwa wanashitakiwa kwa kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.
Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana
wateja wao kwakuwa bado ni watumishi wa serekali na wanao uwezo wa
kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera
Hakimu Mkazi
wa mahakama ya Bukoba Denis Mbelemwa alihairisha kesho hiyo hadi kesho
saa tatu asubuhi baada ya kupitia upya vifungu vya sheria na
kujiridhisha kama watuhumiwa wanasitahili dhamana na kutaka watuhumiwa
warudishwe rumande.
"Nahairisha shauri hili hadi kesho asubuhi
saa tatu nikapitie tena vifungu vya sheria,kutokana na ukubwa wa kesi
hii nione kama watuhumiwa wanadhaminika"alisema
CHANZO: BUKOBA WADAU BLOG
1 comment:
Hivi hawa si ndio wale ubalozi wa Tanzania marekani uliweka crdb account ili watu. Wachangie? Mimi napita tuu na swali la kizushi, hivi ubalozi uli verify vipi information hiyo kabla ya kuutangazia umma?
Post a Comment