Advertisements

Friday, September 2, 2016

YANGA KUPATA UWANJA WA MAZOEZI, NI BAADA YA MANJI KUKODISHWA TIMU NA NEMBOKampuni itakayoingia mkataba na Yanga chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji, itajenga uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini, Francis Kifukwe amethibitisha hilo kwa kusema, kampuni inayokodisha Yanga, imekubali kujenga uwanja wa mazoezi.
“Kweli kila kitu kinakwenda vizuri na baada ya muda fulani, klabu itafanya suala la kuingia makubaliano.


“Suala la uwanja ni kweli, tumekubaliana kuwa lifanyiwe kazi na kampuni hiyo imekubali kujenga uwanja ambao utakuwa sehemu nyingine. Mbali na pale Jangwani ambako sisi tunataka kujenga uwanja wa kudumu.


“Tayari kampuni hiyo imetoa mapendekezo yake, sisi pia tunataka kutoa ya kwetu na kukaa ili kumalizana katika hili,” alisema Kifukwe.

Manji, aliwaomba wanachama wa Yanga moja ya kampuni zake kuikodi nembo na timu ya Yanga kwa kipindi cha miaka 10, jambo ambalo Wanayanga walilipitisha.
CREDIT:SALEHJEMBE

No comments: