Advertisements

Wednesday, October 5, 2016

Aliyetobolewa macho Buguruni Sheli apelekwa Muhimbili

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Jumapili hii aliahidi kumkutanisha Said Ally aliyepoteza uwezo wake wa kuona Buguruni Sheli jijini Dar es salaam, na leo hii amemkutanisha na madaktari wa Muhimbili.


Said Ally amechukuliwa Jumatano hii nyumbani kwake na gari ya mkuu wa mkoa na kupelekwa moja kwa moja katika hospitali hiyo.
Makonda ameandika kwenye Instagram, “Nawashukuru madaktari bingwa kutoka hospitali ya Muhimbili, kwa kazi kubwa wanayoifanya kumsaidia ndugu yangu Said Ally Mrisho apate kuona tena, nawaomba tuendelee kumuombea”, aliandika Makonda.

Mkuu huyo wa mkoa, amejitolea kumsaidia kijana huyo.

BY: EMMY MWAIPOPO

2 comments:

Anonymous said...

Kaz nzuri

Anonymous said...

Allah awasaidie nyote kwa moyo wenu wa upendo. Said pole sana