ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 1, 2016

LIVE UPDATES: Simba vs Yanga Kutoka Uwanja Wa Taifa

MPIRA UMEKWISHAAAA
-Kona ya Yanga, Haji Mwinyi anaruka hapa na kupiga kichwa, nusura aipatie Yanga bao inakuwa gaoal kick

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Simba wanaendelea kushambulia, lakini Yanga hawajalala nao wanajibu mashambulizi
GOOOOOOOOOOOO Dk 87, Simba wanapata kona safi baada ya krosi ya Bukungu. Inachongwana Kichuya,
Dk 85 Juma Abdul krosi yake iipatie Yanga bao baada ya Tambwe kupiga kichwa safi kabisaSUB Dk 81, Msuva anaingia kuchukua nafasi ya Juma Mahadhi
SUB Dk 79, Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Niyonzima.KADI Dk 77, Barthez analambwa kadi ya njano baada ya kuchelewesha muda
SUB Dk 77, Simba wanamtoa Ajib na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim
Dk 76, Kazimoto anageuka na kupiga shuti kali kabisa hapa, lakini ni goal kickDk 74, Simba wanapata kona, inachongwa lakini Yanga wanaokoa kwa ulaini kabisa kupitia Dante hapa
Dk 71, Juuko anaachia mkwaju mkali kwelikweli, mpira unapita juu kidogo kwenye lango la Yanga, goal kick
KADI Dk 71, Twite analambwa kadi ya njano baada ya kumlamba ngwara Kazimoto

KADI Dk 69, Zimbwe Jr analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo
DK 67, Yanga wanapata kona hapa na inakwenda kuchongwa na Haji Mwinyi. Goal Kick, Haji alijaribu shuti lakini limepaa buuu

Dk 64, Tambwe anawachambua mabeki wa Simba na kutoa krosi safi hapa lakini Simba wanaokoa katikati hapa
SUB Dk 62, Simba wanawatoa Lufunga anaingia Juuko Murshid, pia wanamtoa Mavugo na nafasi yake anachukua Blagnon Frederic
Dk 60 sasa, Yanga wanaonekana kutulia zaidi na kucheza taratibu kabisa huku Simba wakionekana kuhaha na hawajatulia kabisa
Dk 58 sasa, timu bado zinashambuliana kwa zamu, Simba wanakuwa na tatizo la kupoteza pasi mara kwa mara
Dk 55 Kazi ipo, Lufunga na Tambwe hapa, Lufunga anampitia Tambwe, yuko chini anatibiwa hapa
Dk 53, Simba wanashambulia, Kichuya anaingia na kupiga shuti kali lakini kuuuubwaaa
Dk 51,, Tambwe yuko chini, inaonekana kama Lufunga alirusha mkono wake ukampata usoni

Dk 50, Zimbwe Jr anafanya kaosa hapa, Kaseke anaingia anapiga kwosri hapa lakini Angban anadaka vizuri
Dk 49, Bukungu anapiga shuti kali ule mpira wa faulo, unagonga mwamba na kurudi, Mavugo anapiga shuti lakini unaokolewa
DK 48, Kichuya anawachambua mabeki wa Yanga, wanamuangusha inakuwa faulo
SUB Dk 47 Yanga inamtoa Yondani na nafasi yake inachukuliwa na Andrew Vicent au Dante
Dk 46, Simba wanaanza kwa kasi, Mwinyi anaingia na kumuangusha Kichuya hapa-


MAPUMZIKO
-Ajibu anawalamba chenga mabeki wa Yanga na kuachia shuti kali lakini ni goal kick
-KADI Yondani analambwa kadi ya njano baada ya kuchelewesha mpira Dakika ya 45 mwamuzi Martin Sanya anapiga filimbi kuashiria mpira ni mapumziko, Yanga 1 na Simba 0.

Dakika ya 44 Simba wanaongeza kujituma lakini shuti la Ibrahim Ajibu linatoka nje na kuwa Goal Kick.

Dakika ya 42 Simba wanapata kona baada ya shambulizi kali lililofanywa na Mavugo na kuokolewa na kipa wa Yanga. Kona inapigwa na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’ na inatoka nje.Dakika ya 41 Yanga wanajibu shambulizi kupitia kwa Mahadhi.

Kichuya anafanya shambulizi lakini umakini unamnyima nafasi ya kuipa timu yake goli la kusawazisha.Dakika ya 36 Donald Ngoma anapiga shuti kali linalodakwa na kipa Angban.

Dakika ya 35 timu ya Yanga wanafanya shambulizi, shuti la Mbuyu Twite linatoka nje.

Dakika ya 30 mpira unaendelea huku mchezaji wa Simba Jonas Mkude kapewa kadi nyekundu baada ya kumtolea maneno machafu mwamuzi

Mpira umesimama Uwanja wa Taifa, baadhi ya mashabiki wa Simba wanakimbia kutoka nje ya uwanja, viti vinaendelea kung’olewa upande waliokaa mashabiki wa Simba.

Dakika ya 26 Amis Tambwe anawainua mashabiki wa Yanga anafunga goli la kwanza.

Dakika ya 24 mchezaji Amis Tambwe anafanya faulo na mpira unapigwa kuelekea lango la timu ya Yanga, mpira unatoka nje.
Kelvin Yondani anaongoza ukuta wa Yanga unaokaba kwa kutumia nguvu na umakini, mchezo umejaa kila aina ya ufundi kutoka pande zote mbili.

Yanga wanacheza kwa umakini wa hali ya juu wakikaba kwa pamoja na wanaposhambulia wachezaji wote wanapanda kusaidia..

Dakika ya 16 Yanga wanajipanga na kuingia kwenye eneo la hatari kwa ushirikiano wa Tambwe, Ngoma, Mahadhi… Off side.Dakika ya 11 mchezaji wa Simba, Mavugo anafanyiwa rafu na kutolewa nje kutibiwa.

Dakika ya 09 Mavugo anapiga mpira wa faulo na kugonga ukuta wa mabeki wa Yanga.

Yanga wanapata kona ya kwanza kwa makosa ya beki.

Kikosi cha timu ya soka ya Simba wameanza kwa kasi kupitia kwa wachezaji wao Kichuya, Mavugo na ajibu bado timu zote zinaviziana.

Mpira umeanza saa kumi kamili. Timu ya Simba wakiwa wamevaa jezi zao za rangi nyekundu na Yanga wamevaa jezi za rangi ya kijani.
kikosi cha timu ya Simba.
kikosi cha timu ya Yanga.
Viongozi Mbalimbali wakiwa tayari uwanjani kuangalia pambano hilo.

Picha ba habari kwa hisani ya GPL na SalehJembe Blog

No comments: